24.8 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

Benkiya NMB yatoa misaada ya milioni 17.3 kwa shule nne Mufindi

Na MwandishiWetu, Mufindi

Benkiya NMB imetoa misaada ya vifaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 17.3 kusaidia kuboresha upatikanaji wa huduma za jamii katika Wilayani Mufindi.

Kaimu Afisa Tawala Wilaya ya Mufindi – Joseph Mchina akimkabidhi Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Isupilo, Patrick Mwageni msaada wa Meza kwa ajili ya Walimu zilizotolewa na Benki ya NMB Kanda ya Nyanda za Juu. Wengine ni Meneja wa NMB Mufundi – Mary Mpasha (Kushoto mwenye miwani) na Katikati ni Meneja wa NMB Nyanda za Juu – Straton Chilongola (Miwani).NMB ilitoa madawati, Mabati kwaajili ya shule nne za msingi vyenye thamani ya Sh Milioni 17.3

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na madawati 50 kwaajili ya shule ya Msingi Upendo, Viti 12 na meza 12 kwaajili ya shule ya Isupilo na Mabati 200 kwaajili ya shule za msingi Nyamalala na Amani yenye lengo la kuezekea madarasa vyote vikiwa na thamani ya Sh milioni 17.3.

Baada ya kupokea misaada hiyo, Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Joseph Mchina, aliishukuru NMB kwa kuendelea kuchangia shughuli za maendeleo wilayani humo.

“Misaada hii imekuja wakati muafaka kwani itasaidia sana kupunguza uhaba wa madawati kwa shule zetu na pia kukamilisha baadhi ya madarasa ambayo yalikuwa ymameshajengwa lakini nguvu zilikuwa zinahitajika katika kuezeka, nawashukuru sana NMB,” aisema Mchina.

“Benki ya NMB imekuwa maili kwenye kuunga mkono juhudi za maendeleo za wananchi na kuisaidia Serikali kuboresha huduma za jamii. Naguswa na jinsi mnavyoe ndelea kutushika mkono sisi watu wa Mufindi na tunaomba msichoke kutusaidia,” alisema.

Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Joseph Mchina akimkabidhi Meza na Madawati 50 Mkuu wa shule ya Sekondari Upendo – Judith Kisoma mara baada ya kupokea msaada huo kutoka Benki ya NMB Kanda ya Nyanda za Juu,Wengine katika Picha ni Meneja NMB Kanda ya Nyanda za Juu, Straton Chilongola(katikati)Meneja wa NMB Tawi la Mafinga, Mary Mpasha (kushoto) na Manaja Mahusiano ya serikali kutoka Benki ya NMB Kanda Nyanda za Juu- Humprey Kaaya(kulia).

Mchina alisema kuwa ifike wakati wananchi waone umuhimu wa benki ya NMB katika kujitoa kwao na zawadi pekee ni kuwaunga mkono katika kufungua akaunti na kutumia benki hiyo kuweza kupata faida zaidi ili nao watoe zaidi kwa jamii katika sekta mbalimbali.

Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu – Straton Chilongola aliushukuru uongozi wa wilaya kwa juhudi zake za maendeleo ya wananchi amba alisema ni wadau wakubwa kwa mafanikio ya benki ya NMB.

Alisema pia NMB inatambua mchango wa serikali kwenye kuisaidia kuweka mazingira wezeshi ya biashara wilayani Mufindi na hvyo na kwa mantiki hiyo nayo itaendelea kuwekeza kwa namna mbalimba ili kuwawezesha wananchi ambao ndio wadau wakubwa wa benki ya NMB kibiashara.

Aliongeza kuwa changamoto za sekta ya elimu na afya kwa NMB ni jambo la kipaumbele linalo hitaji kuunganisha nguvu kulikabiri.

“Ingawa Serikali inafanya makubwa, sisi kama wadau tuna wajibu wa kuunga mkono juhudi hizi za maendeleo kwa kusaidia jamii kwani kupitia jamii hiihii, ndio imeifanya Benki ya NMB kuwa hapa ilipo na kubwa kuliko benki yoyote hapa nchini.

“Sisi kama NMB tumekuwa mstari wa mbele kuchangia huduma za jamii kwa lengo la kurejesha sehemu ya faida yetu kwa jamii. Kwa zaidi ya miaka 10 mfululizo tumekuwa tukichangia asilimia moja ya faida yetu kila mwaka kama sehemu ya uwajibikaji kwa jamii inayo tuzunguka,” amesema Chilongola.

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Upendo iliyopo Mafinga Wilayani Mufindi wakiwa wamesimama nyuma ya Madawati 50 ambayo yametolewa msaada na Benki ya NMB Kanda ya Nyanda za Juu.

Wanafunzi washule zilizosaidiwa walisema msaada waliopata ni motisha tosha ya wao kufanya vizuri kitaa luma. Walimu wakuu wao walisema mchango wa NMB si tu nisehemu ya kurudisha fadhira kwa jamii lakini pia ni mchango mkubwa katika juhudi za kuboresha elimu nchini.

Chilongola aliongeza kuwa NMB inatambua juhudi za serikali kusimamia elimu na afya kwa nguvu zote kwa kutoa elimu bila malipo kwa shule za msingi na sekondari na kuboresha huduma za elimu na afya mjini na vijijini hivyo kama wadau kuna wajibu wa kuunga mkono juhudi hizo za maendeleo kwa jamii kwani ndio wameifanya benki ya NMB kuwa ilipo na kuwa benki kubwa kuliko zote nchini.

Meneja wa benki hiyo Tawi la Mafinga, Mary Mpasha alisema kuwa ushirikiano unaotolewa unasababisha biashara ya NMB kukua zaidi hivyo kufanya kama benki kuweza kutoa faida kwa jamii inayowazunguka kama benki bora nchini kwa sasa na yenye matawi mengi zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,264FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles