27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Benki ya Ushirika Kilimanjaro yatenga milioni 500 ya mikopo

Na Upendo Mosha, Moshi

Benki ya Ushirika mkoani Kilimanjaro (KCBL) imetenga zaidi ya Sh milioni 500 kwa ajili ya mikopo ya bajaji na pikipiki bila riba kwa vijana kwa lengo kuongeza frusa ya ajira na kupunguza changamoto ya ajira.

Hayo yalibainishwa na Mkuu wa kitengo cha Biashara na Mikopo wa benki hiyo, Mbaraka Biabato, wakati wa uzinduzi wa mkopo huo wa wajasiriamali na waendeshaji wa vyombo vya moto aina ya bajaji,Jana Mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

Alisema benki hiyo imefikia maamuzi ya kutenga kiasi hicho cha fedha kwaajili ya ununuzi wa bajaji zaidi ya mia moja ambazo zitalolewa kwa makundi ya wajasiriamali na vijana jambo ambalo litapunguza changamoto ya ukosefu wa ajira na kujikwamua kiuchumi.

“Tumetenga zaidi ya milioni mia tano kwaajili ya kuwakopesha makundi ya wajasiriamali na vijana, tunataka wamiliki bajaji zao wenyewe jambo hili litawasaidia kujikwamua kiuchumi jambo wanalopaswa kufanya ni kufungua akaunti na kuwekeza Sh milion 2.5 tu,” alisema Biabato.

Aidha alisema tayari benki hiyo imekwishatoa mikopo ya bajaji hizo kwa baadhi ya vijana na makundi ya wajasiriamali na kwamba ni muda muafaka kwa vijana na wajasiriamali kuchangamkia fursa hiyo iliyolenga kuondoa umasikini kwa jamii.

“Tunaimani kuwa ifikapo mwenzi Desemba Mwaka huu tutakuwa tumeshatoa mkopo wa bajaji zaidi ya nusu kwa vijana wasiriamali wa mkoa wa Kilimanjaro…lengo letu ni kubadilisha maisha ya watanzania ambao ni vijana tunataka waondoke kwenye magenge ya uhalifu na uuzaji wa dawa za kukevya na wafanye kazi halali,” alisema Biabato.

Alifafanuazaidi kuwa kwa wiki watakuwa wanarejesha Sh 86,400 ambacho ni kiasi kidogo ikilinganishwa na huko walipo ajiriwa ambapo wanapeleka 120,000 kwa wiki ambazo ni nyingi na haitoi frusa ya kujikwamua kiuchumi,” alisema.

Akizindua mkopo huo,Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi,Juma Raibu, aliwataka vijana hao kuwa waaminifu katika urejeshaji wa mkopo huo na kuacha kutumia bajaji hizo kusafirisha dawa za kukevya aina ya mirungi.

“Mkopo huu Ni kwajili yenu tumieni frusa hii vizuri Ila niwaonye msije mkatumia bajaji kufanyia uhalifu maana mtapoteza maana ya mkopo huu, pia mkafuate sheria za barabarani kiwa ni pamoja na kulipa madeni yenu ya maegeshilo ya bajaji mpaka Sasa tunadai bajaji zaidi ya 1,000 Kati ya 2,500 zilizopo katika manispaa yetu,”alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles