30.5 C
Dar es Salaam
Monday, December 6, 2021

Benki ya UBA yazindua shughuli Uingereza

Mwandishi Wetu

Benki ya UBA imezindua shughuli zake nchini Uingereza na kutambulishwa rasmi kwa viongozi wa kibiashara kutoka Ulaya na Afrika.

Hafla hiyo ya uzinduzi ilifanyika nchini humo wiki iliyopita ikiwa ni wiki chache baada ya kuzindua shughuli zake nchini Mali ambapo lengo ni kuchochea biashara baina ya mabara hayo.

Hatua hiyo inaiweka benki hiyo kuwa moja kati ya sekta za kibenki na taasisi ya kwanza na pekee ya kifedha kusini mwa jangwa la Sahara Afrika inayoendesha shughuli nchini Uingereza na Marekani.

Akizungumza katika tukio hilo, Mwenyekiti wa UBA Group, Tony Elumelu, alisema benki imefurahishwa na mamlaka za Uingereza kuiruhusu kuimarisha na kupanua operesheni zake na hivyo kutimiza dhamira yake ya kupanua biashara na uwekezaji baina ya Afrika na Ulaya.

“Furaha yangu ni kuona UBA kama benki kutoka Afrika inavyoweza kuchomoza na kusaidia wawekezaji katika miji muhimu ya kifedha duniani,” alisema.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa UBA Group, Kennedy Uzoka, alisema benki hiyo inahudumia mahitaji ya kibiashara na mitaji kwa wateja wa Afrika, ambao wanatafuta masoko Ulaya.

“Kwa kuzindua UBA UK Limited, tunafurahi kupanua huduma hizo kwa wateja wa sasa, wakati huo huo tukikaribisha wapya waweze kikamilifu kutimiza ndoto zao za kifedha kupitia mtandao wetu wa kibenki,” alisema.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,263FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles