29.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 19, 2022

Benki ya Posta yatoa stika za usalama barabarani

24Na Hadia Khamis -DAR ES SALAAM

BENKI ya Posta Tanzania (TPB), imetoa msaada wa stika zaidi ya 2,000 zenye namba za wakuu wa usalama barabarani wa mikoa yote nchini zitakazobandikwa kwenye mabasi yaendayo mikoani.

Akizungumza wakati wa kubandika stika walizozipokea katika mabasi hayo mwishoni mwa wiki, Kamanda Mkuu wa Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga, aliwataka madereva  kuendelea kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani ili kutokomeza ajali zinazoendelea kupoteza maisha ya watu wengi.

Alisema ofisi yake ilikuwa inapokea maombi mengi kutoka kwa wananchi ili kupata namba zitakazowawesha kutoa taarifa za madereva wanaofanya makosa wakiwa safarini.

Alisema stika hizo zitabandikwa katika mabasi yote yaendayo mikoani pamoja na yale madogo maarufu kama Coastal.

“Tunaishukuru Benki ya Posta kwa msaada huu kwani wametupa muda mwafaka wa kuelekea mwishoni mwa mwaka ambapo kumekuwa na ajali nyingi sana zinazopoteza maisha ya watu wengi na kuwaacha wengine na ulemavu wa kudumu,” alisema Kamanda Mpinga.

Aliongeza kuwa kitengo chake kitaendelea kushirikiana na TPB na wadau wengine kuhakikisha wanaendesha kampeni hii na kutokomeza kabisa ajali za barabarani.

Akikabidhi msaada huo, Meneja Masoko na Uendeshaji wa TPB, Deo Kwiyukwa, alisema lengo la kutoa stika hizo ni kupunguza ajali na kupoteza nguvu kazi ya taifa katika kipindi hiki cha kuelekea mwishoni mwa mwaka.

Alisema kwa kipindi cha miaka minne iliyopita toka waanze kampeni hiyo, ajali zimepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na madereva kuhofia kuripotiwa na abiria katika vyombo vya usalama ambapo itapelekea kusimamishwa, faini kali au kifungo.

“TPB tunapenda kuwaasa watumiaji wa mabasi ambao wengi ni wateja wetu kutoa taarifa katika vyombo vya usalama pale madereva wanaofanya makosa hasa,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,987FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles