25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

BENKI YA POSTA YAFANYA MABADILIKO MAKUBWA

Na FERDNANDA MBAMILA-DAR ES SALAAM


WAKATI  Serikali  ya Tanzania  ilipotoa tamko la kuyataka  makampuni  na mabenki   mbalimbali nchini ambayo yalikuwa bado hayajasajiliwa  rasmi yajisali ifikapo mwaka  2017, hatimaye Benki ya Posta (TPB Plc)  imeshakamilisha  zoezi hilo.

Kutokana na usajili huo, benki hiyo imeweza kubadili nembo yake ya awali na  sasa imebadilika na kutumika kuanzia   Januari 19, mwaka huu na jina lake kuwa TPB Plc.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPB Plc,  Sabasaba Moshingi,  anasema mabadiliko hayo  yanakwenda  sambamba na mabadiliko  makubwa yanayotokea ndani ya benki  hiyo. 

Anaendelea kusema kuwa mabadiliko ya kibenki yalianza kutekelezwa toka mwaka  2001  kwa kuanza na kuchagua upya  viongozi  lakini kwa bahati nzuri, ninashukuru  Mungu nilichaguliwa na mpaka leo nipo katika kitengo hiki.

“Vilevile tulibadilisha mwonekano wa  matawi  zaidi ya 28  hapa nchini na kuwa ya kisasa  katika mikoa mbalimbali, tulibadilisha mfumo wa utoaji wa huduma  kwani kwa kipindi hicho tulikuwa katika benki nyingi, vilikuwa vikitumika vitabu lakini ni tofauti na sasa kwani kuna teknolojia mahususi ambayo hutumika zaidi katika mabenki mengi,” anasema

Pia anasema TPB wameimarisha huduma ya kibenki  kwa njia ya simu  kutoka kwenye  benki na  kwenda katika simu ya kiganjani (simbankig).

Anasema kuna huduma nyingine nyingi ambazo wameziunganisha kwa ajili ya kinamama, mojawapo ni njia ya vicoba,  kwa maana hiyo badala ya kuweka fedha katika vibubu wana uwezo wa kuhifadhi benki.

“Benki hiyo imeweka mfuko wa wastaafu  wa wafanyakazi  iliyokuwa Posta kiasi cha Shilingi bilioni 77, pia  imejenga nyumba katika Mkoa wa Njombe  kwa ajili ya watu wasiojiweza,” anasema  Moshingi.

Anasema  benki yake imekamilisha mchakato wake wa muda mrefu  wa kuisajili benki hiyo  chini ya sheria ya kampuni, ambapo mchakato huo ulikamilika toka mwaka jana  na hivi sasa benki hiyo inaitwa  TPB Bank plc.

“Benki iliamua kuanzisha  kubadilisha nembo  yake  ili  kwenda sambamba na jina hilo  pamoja na mabadiliko  makubwa  ya kuiboresha benki hii yanayoendelea,” anasema  Moshingi.

Aliishukuru  sana  Wizara ya fedha  kwa ushirikiano huu  kuzidi kuendelea baina yao  hususani katika kipindi hiki ambapo  benki ipo  katika  mchakato wa  kuingia katika soko la hisa.

Anasema  lengo na madhumuni hasa ni  kupata mtaji  ili benki iweze kujiendesha  yenyewe kwa ufanisi zaidi.

Naye Mwenyekiti wa Bodi  ya wakurugenzi  wa TPB  Plc, Prof. Lettice Rutashobya,  alimhakikishia Waziri  wa Fedha kuwa  benki hiyo  itaendelea kutoa huduma bora kwa  wateja wake ili kufikia maendeleo zaidi.

Prof. Rutashobya anasema  vilevile  ataweka jitihada zaidi ili kuwafikia Watanzania wengi  hususani wale walioko  pembezoni ili nao waweze kufaidika na huduma za kifedha  zinazotolewa na benki hiyo.

“ Ingawa tuna changamoto ya mtaji wa kutosha wa kuwafikia wananchi, asilimia 14 pekee ndiyo huduma iliyowafikia wananchi katika benki yetu lakini,” anasema  Prof. Lutashobya.

Anasema tumeanza mchakato wa kuungana na benki nyingine nchini kwa lengo la kuikuza na kuiendeleza benki yetu ili iweze kuwa juu zaidi kimaendeleo.

Uzinduzi huo  ambao ulifanywa na Waziri wa  Fedha na Mipango, Dr. Phillip Mpango na kuhudhuriwa na baadhi ya viongozi  mbalimbali nchini na  Waziri  aliupongeza  uongozi wa benki kwa  hatua waliyofikia ya kuweza kuthubutu katika kuikuza na kuiendeleza benki hiyo.

Anasema: “Nimeona baadhi ya benki nyingi nchini zimeendelea kukua  kimaendeleo kwa utoaji wa huduma  za kibenki kwa wananchi.

“Kitu ambacho kimenivutia zaidi katika benki zote ni kuongezwa kwa mashine za kutolea fedha, yaani (ATM) na huduma za simu.

“ Serikali inamini kuwa  katika maendeleo ya miaka hii katika kuanzisha viwanda vidogo vidogo na vya kati,  ili tuwe na Tanzania ya viwanda,” alisema  Mpango.

Vile vile Mpango anasema matarajio ya Serikali kwa makampuni na benki zote nchini ni kupitia huduma hiyo  kuwafikia wananchi hadi vijijini.

“Kama tatizo ni mtaji inabidi mjitahidi zaidi kwa hali na mali kutafuta vyanzo  mbadala ambavyo  vitawezesha upatikanaji wa mtaji huo ili kuweza kuwafikia wananchi kwa urahisi zaidi,” anasema Mipango.

Anasema wakifanya hivyo watakuwa wazalendo wakubwa nchini kwa kuanza na nyumbani kwanza, kwa kununua vya kwao.

Hata hivyo, aliwaomba Watanzania  wote kuwa na huduma hii itakapofika sokoni kuuza hisa kwamba Watanzania wawe wa kwanza  kununua hisa hizo.

 “Katika suala la mtaji nina imani tutaendelea  kulifanyia kazi  kwa kushirikiana kwa pamoja ili tuweze kufanikisha na wananchi waweze kufaidika,” anasema Mpango.

Vile vile ameiasa bodi ya benki hiyo kutengeneza  utaratibu wa  kutoa  mikopo kwa wananchi  ili kuongeza wigo wa utoaji wa huduma.    

Anasema” Sisi kama Serikali  tutaendelea  kutoa ushirikiano  kwenu ili hatimaye benki hii ijiimarishe  kimtaji na kuweza  kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

“Nimefarijika sana  kusikia  kuwa benki hii imefanikiwa  kwa kupeleka huduma zake za kibenki hadi pembezoni mwa nchi,  kwa kujenga  matawi  yenu kwenye miji mikuu karibu yote nchini pamoja na  kufikisha huduma yenu  ya TPB popote,” anasema  Dk. Mpango.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles