28.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Benki ya NMB yajizatiti kuwezesha wafanyabiashara kuchangamkia fursa kwenye miradi ya kimkakati

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Benki ya NMB imesema ipo tayari kutoa fedha kuwezesha wafanyabisahara wakubwa, wakati na wadogo kuchangamkia fursa kwenye miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwemo miradi ya bomba la mafuta na mradi wa reli wa SGR ikiwa ni juhudi za benki hiyo kuchangia maendeleo ya Tanzania.

Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NMB, Christopher Mgani, akifafanua jambo kwa wadau kuhusu Bidhaa za Benki hiyo wakati wa hafla fupi iliyokutanisha wadau wa Mafuta na Gesi na kufanya majadiliano, iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana ambapo Benki ya NMB ilikuwa ni miongoni mwa wadhamini.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Mifumo ya Miamala wa Benki ya NMB, Linda Teggisa, amesema benki yake inatoa hadi bilioni 326 (sawa na dola milioni 140) kwa mkopaji mmoja.

Akizungumza katika hafla ya jioni iliyoandali wa mwamvuli wa Watoa Huduma kwenye Sekta ya Mafuta na Gesi (ATOGS) jijini Dar es Salaam ljuma jioni , Teggisa alisema benki yake inatambua mahitaji ya wafanyabiashara wanaoshiriki katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati na ndio maana ilikuja na suluhishi mahususi zinazolenga mahitaji yao na mnyororo wa kuongeza thamani kama usafiri, bima na uzalishaji.

 “Benki ya NMB imejipanga kutoa mchango mkubwa wa kifedha kuwawezesha wafanyabiashara wakubwa, wa kati na wadogo ili waweze kuchangamkia fursa mbalimbali kwenye miradi ya kimkakati na sekta ya  nishati, mafuta na gesi. Kama benki, nia yetu ni kuhakikisha kuwa Watanzania wanashiriki kikamilifu bila  vikwazo vya fedha,” alisema.

Teggisa alisema kuwa hadi mwezi huu, benki yake imetoa kiasi cha bilioni 469.9 kama mikopo kwa wadau mbalimbali kwenye sekta ya mafuta na gesi. 

“Tutaendelea kotoa huduma za kibenki zinazoendana na mahitaji ya soko la sasa katika harakati zetu za kuchangia maendeleo ya taifa letu. Pia tumeweza kuja na mifumo inayowezesha malipo ya serikali kupitia mfumo wa GePG  ili kuwezesha malipo ya kodi na huduma mbalimbali ya serikali.

Kwa upande wake Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Biashara Christopher Mgani aliwasihi wafanyabisahara nchini kuchangamkia fursa ya Bancassurance inayotolewa na benki hiyo ili kupunguza hatari kwenye biashara zao.

“Kupitia huduma yetu ya  Bancassurance, mfanyabiashara atafanya  biashara yake kwa uhuru kwa kuwa huduma hii  inampatia bima ya kujikinga na majanga mbalimbali ikiwemo uharibifu wa mali, afya na tayari tumejiunga na makampuni 10 nchini kutoa huduma hii nchi nzima,” alisema.

Naye mwenyekiti wa Bodi ya ATOG Abdulsamad Abdulrahim wakati wa hafla aliishukuru  benki ya NMB kwa uzalendo kwa jitihada zake za kuchangia miradi mbalimbali ya kimkakati, nishati, mafuta na gesi. 

 “Tunaishukuru benki ya NMB kwa kuja na huduma za kibenki zinazolenga kusaidia wafanyabiashara mbalimbali. Benki hii imeenda mbali kwa kurekebisha masharti hasa kwenye upande wa dhamana. Hiki kilikuwa kilio cha wafanyabiashara wengi kwa miaka mingi na tunaishukuru benki kwa kuona mbali na kilifanyia kazi jambo hili,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles