26.1 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Benki ya NCBA yakabidhi maliwato ya kisasa kwa Klabu ya Gofu Lugalo

Dar es Salaam,

Benki ya NCBA Tanzania Limited imekabidhi maliwato ya kike kwa wachezaji wa klabu ya Gofu ya Lugalo jijini Dar es Salaam jana.

Akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano hayo, Mkurugenzi wa Biashara na Huduma za Kidigitali wa benki hiyo, Gift Shoko amesema benki hiyo ipo kwa ajili ya kurudisha kwa jamii kile wanachokipata ili kiwezeshe kunufaisha jamii

Pia ameshukuru wadau wenzake Resolution Insurance na GardaWorld kwa kuwezesha kufanikisha dhamira yetu kwa wachezaji wa kike wa klabu hii. alimaliza kusema Bw.Shoko

Kwa upande wake Mwenyekiti wa klabu hiyo, Brigedia Jenerali Mstaafu, Michael Luwongo ameishukuru benki ya NCBA na wahisani wengine kwa kufanikisha ukarabati wa Maliwato hiyo na kuwa ya kisasa na kusema kuwa itawafanya kinamama sasa kabla na baada ya mazoezi waweze kwenda kubadilisha nguo bila hofu ya mazingira, tofauti ilivyokuwa awali.

“Ninamini NCBA Bank kupitia kwa rafiki yangu Gift Shoko watasaidia mambo mengi kwenye klabu yetu hii na niwaombe wadau wengine waige mfano ulionyeshwa na benki hii mpya nchini,” amesema Luwongo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,734FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles