Na Asha Bani, Mtanzania Digital
WASTAAFU na Wafanyabiashara wadogo wadogo nchini wanatanufaika na mikopo katika benki ya Letshego baada ya kuweka akiba kuanzia kiasi cha Sh 1,000.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo Septemba 27, Mkuu wa kitengo cha Mauzo wa benki hiyo, Leah Phili amesema lengo ni kufikia wajasiriamali wengi ifikapo mwisho wa mwaka.
Amesema kwa kufanikisha hilo Letshego imefungua akaunti mbili moja ya mjasiriamali na nyingine ya mstaafu ambapo watahakikisha wananufaika na akaunti hiyo kwa kujikwamua na umaskini.
“Akaunti hizo zitawanufaisha wateja wao na pia tunamalengo ya kuwafikia wafanyabiashara wadogo 900 na wastaafu 300 na hakuna masharti zaidi ya kuwa na kitambulisho cha uraia,” amesema Leah.
Amesema huduma hizo zinapatikana katika matawi yao yote yaliyopo Dodoma, Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na maeneo mengine.
Ameongeza kuwa mfanyabiashara mdogo anaanzia kujiwekea akiba kuanzia shilingi 1000 na kuendelea na kuweza kukupa kuanzia shilingi 200,000 na kuendelea.