28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

BENKI YA KILIMO KUTOA MIKOPO RAHISI KWA WAKULIMA

CHRISTINA GAULUHANGA Na TUNU NASSOR


BENKI ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), imesema itaendelea kushirikiana na benki za biashara ili kufikisha mikopo kirahisi kwa wakulima nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara, Mkurugenzi wa Fedha na Tehama wa TADB, Severin Ndaskoi, alisema  kwa kuwa ni wachanga, hawawezi kwa haraka kufanya uwekezaji katika kila mkoa.

Alisema ili lengo la kuwainua wakulima liweze kutimia, ni vyema wakashirikiana na mabenki kuwawezesha wakulima.

“Kilimo hakina dhamana hivyo mabenki mengi yamekuwa yakiogopa kupoteza fedha endapo mkulima atapata hasara, hivyo ili TADB itimize lengo lake, tumekuwa tukishirikiana na wakulima ambapo wenzetu hutoa asilimia 50 ya mikopo na sisi hivyo hivyo,” alisema Ndaskoi.

Ndaskoi alisema benki hiyo ilianza na mtaji wa Sh bilioni 11 hapa jijini Dar es Salaam, ambapo changamoto kubwa ilikuwa ni uhaba wa wakulima hapa jijini.

Alisema mwaka 2016 walianza na Sh bilioni 2, ambapo mwanzoni mwa mwaka huu ilikuwa Sh bilioni 11 na sasa imefikia Sh bilioni 45.

“Hadi kufikia mwaka huu, tutakuwa na Sh bilioni 120 kwa ajili ya mikopo ya wakulima,” alisema Ndaskoi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles