28.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

BENKI YA DUNIA YAIPONGEZA TANZANIA  MATUMIZI YA FEDHA

Na FARAJA MASINDE-ALIYEKUWA BAGAMOYO


BENKI ya Dunia (WB) imesema Tanzania ni moja ya nchi barani Afrika ambayo inatumia vizuri fedha za miradi inayofadhiliwa na benki hiyo kwa kushirikiana na Serikali.

Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Kiongozi wa WB anayeshughulikia miradi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf), Mohammed Mderis.

Aliyasema hayo  baada ya kutembelea miradi mbalimbali mkoani Pwani ambayo inasimamiwa na mfuko huo kwa lengo la kunusuru kaya masikini.

“Ni jambo la faraja kuona fedha zinazotolewa Tanzania  na Benki ya Dunia zinatumika vizuri na zimeleta mabadiliko chanya katika maisha ya wanachi.

“Ukitazama kwa Afrika, Tanzania imekuwa ni namba moja kwa kutumia vizuri fedha hizi jambo hili ambalo limetupa moyo,” alisema Mderis.

Naye  Mkurugenzi wa Uhusiano wa Nje wa benki hiyo, Heleh Bridi alisema kulingana na miradi aliyotembelea na ushuhuda mbalimbali alioupata  kutoka kwa wananchi wa kaya zinazonufaika, ni wazi fedha wanazotoa ziko kwenye mikono salama.

“Tumejionea wenyewe kwa wananchi kupitia ushuhuda wa maisha yao, hata miradi wanayofanya ni wazi fedha zetu ziko kwenye mikono salama na hii imetupa moyo wa kuendelea kushirikiana na Tanzania.

“Kubadilisha maisha ya zaidi ya Watanzania milioni moja  kutoka kwenye umaskini ni jambo la kujivunia.

“Tunaishukuru Serikali ya Tanzania kuendelea kuunga mkono mpango huu, umekuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo ingawa kuna changamoto ndogo ndogo ikiwamo kubadilisha mfumo wa utoaji fedha kwa wananchi kutoa njia inayotumika hivi sasa ya kukabidhi fedha mkononi na kutumia mfumo wa elektroniki,” alisema Bridi.

Bridi aliitaka Tasaf kuendela kusimamia vema miradi hiyo ikiwamo pia kuongeza ukaribu na wanufaika  kusikiliza changamoto zinazowakabili.

Alisema WB itaendelea kufadhili mpango huo hadi 2019.

“Kama wafadhili wakuu wa mradi huu tuko tayari kuendelea kuufadhili kwa kiwango kikubwa zaidi, tukileta washirika wengine kama Shirika la Maendeleo la Canada (CIDA) na wengine  kusaidia kaya nyingi zaidi kufikiwa na kuondokana na umasikini,” alisema Bridi.

Mradi wa Tasaf unanufaisha kaya milioni 11 nchini na  hadi kufikia Desemba mwaka jana, Sh bilioni 431 zilitumika kulipa wanufaika wa mpango huo ulioko awamu ya tatu sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles