26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Benki ya Akiba yatoa gawio kwa wanahisa

Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Akiba, Israel Chasosa
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Akiba, Israel Chasosa

Na MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

BENKI ya Akiba imetangaza gawio la Sh 75 kwa hisa kwa wanahisa wake kwa mwaka unaoishia Desemba 31, 2015.

Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Akiba, Israel Chasosa, alisema hilo ni ongezeko la zaidi ya asilimia 100 ikilinganishwa na gawio la Sh 30 kwa hisa lililotolewa mwaka 2014.

Chasosa alisema kutolewa kwa gawio hilo ni matokeo ya benki hiyo kufanya vizuri katika biashara ikiwamo kupata faida tangu  kuanzishwa kwake miaka 18 iliyopita.

“Wakati wa kuamua ulipaji wa gawio, bodi ya benki yetu huangalia zaidi uwiano kati ya gawio hilo na kubakiza faida nyingine  iweze kurudishwa kwenye uendeshaji wa benki kwa ajili ya kukuza biashara,” alisema.

Chasosa alisema hiyo ni mara ya tatu mfululizo kwa benki hiyo kutoa gawio kwa wanahisa wake.

“Hii ni ishara kwamba wanahisa wetu wana imani kubwa na benki yetu kwa vile  tumekuwa tukipata faida endelevu kwa muda wote ambao tumekuwa kwenye biashara,” alisema.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2015 iliyokaguliwa, benki hiyo ilipata faida ghafi ya Sh bilioni 5.3 mwaka jana, ambako kiwango kama hicho kilipatikana   mwaka 2014.

Ripoti hiyo inaonyesha kwamba  katika kipindi cha mwaka 2015 benki hiyo ilitoa mikopo ya Sh bilioni 107.3 ikilinganishwa na Sh bilioni 77.2 zilizokopeshwa mwaka 2014.

Rasilimali za benki ziliongezeka hadi kufikia Sh bilioni 163.7 mwaka 2015 ikilinganishwa na Sh bilioni 135.3 kwa mwaka 2014 wakati mtaji wa benki ulikuwa na kufikia Sh bilioni 19.3 mwaka jana kutoka Sh bilioni 16 mwaka 2014.

Pato kwa kila hisa lilikuwa ni Sh 466 mwaka jana ikilinganishwa na Sh 400 mwaka 2014.

Chasosa alisema mwaka 2015 ulikuwa mwaka wa mageuzi makubwa kwa benki hiyo kwa sababu   ulikuwapo  ubunifu mkubwa ambao ulisababisha bidhaa na huduma zake kuongezeka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles