26.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 24, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Benki ya Akiba yakabidhi zawadi washindi kampeni ya twende kidigitali

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wateja sita wa Benki ya Akiba (ACB) kutoka matawi mbalimbali wamekabidhiwa zawadi za fedha taslimu pamoja na nyingine baada ya kuibuka washindi wa kampeni ya Twende Kidijitali – Tukuvushe Januari.

Akizungumza Februari 14,2025 wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi hizo, Ofisa Biashara Mkuu wa Akiba Commercial Bank, Wezi Mwazani, amesema kampeni hiyo imelenga kuwahamasisha wateja wa benki kutumia huduma za kidijitali kwa urahisi zaidi kwa kuwa zinaboreshwa pia upatikanaji wa huduma za kifedha na kuongeza usalama wa miamala.

Washindi hao walipatikana kwa kuangalia matumizi yao makubwa ya huduma za kidijitali, zikiwemo ACB Mobile, Internet Banking, na VISA card hivyo amewapongeza na kuwashukuru kwa kushiriki katika kampeni hiyo.

“Tunawapongeza washindi wetu kwa kuwa sehemu ya safari yetu ya kidijitali. Kupitia huduma kama ACB Mobile, Internet Banking, na VISA card, wateja wetu mmeweza kufanya miamala kwa haraka, ikiwa na usalama na kwa urahisi zaidi tunawahamasisha wengine kuendelea kutumia huduma hizi kwa manufaa yao,” amesema Wezi.

Baadhi ya washindi wa kampeni hiyo wamefurahishwa na hatua ya benki kutambua matumizi yao ya huduma za kidijitali kwa zawadi na wamepata uzoefu wa kutumia huduma hizo huku wakiahidi kuendelea kuzitumia.

Kampeni ya Twende Kidijitali – Tukuvushe Januari ni sehemu ya mkakati wa Akiba Commercial Bank wa kuhamasisha matumizi ya huduma za kidijitali ili kuwapatia wateja wake suluhisho bora na la kisasa katika upatikanaji wa huduma za kibenki popote walipo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
595,000SubscribersSubscribe

Latest Articles