29.8 C
Dar es Salaam
Monday, October 7, 2024

Contact us: [email protected]

Benki ya Akiba sasa kusogeza huduma zaidi mtaani

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Taasisi za kifedha zimeshauriwa kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wananchi kwa kuwasogezea karibu na kuwapunguzia adha ya kutumia muda mwingi na umbali mrefu.

Wito huo umetolewa Septemba 21, 2024 Dar es Salaam na Kaimu Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Biashara Benki ya Akiba, Danford Muyango, wakati akizindua kampeni ya benki hiyo inayolenga kusogeza huduma karibu na wananchi ijulikanayo kama ‘Tupo Mtaani Kwako’.

Amesema wapo mtaani kutoa huduma ikiwemo elimu ya mikopo, jinsi ya kutumia huduma za kidigitali VISA card, ACB Mobile, Akiba Wakala na Internet Banking.

”Tumezindua rasmi programu yetu ya Tupo mtaani kwako kupitia timu yetu bobezi ya mauzo, sasa tunawafikia wananchi popote walipo nchi nzima. Kupitia timu yetu ya mauzo watapata huduma za kufungua akaunti, elimu ya mikopo na jinsi ya kutumia huduma za kidijitali za VISA card, ACB Mobile, Akiba Wakala na Internet Banking,” amesema Muyango.

Muyango amesema programu hiyo inaenda sambamba na kampeni ya Road show ya kutoa utambulisho kwa timu ya ‘Tupo Mtaani kwako’ katika vitongoji na mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles