26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Benki UBA Plc yatangaza safu ya vigogo wake

* Oliver Alawuba ateuliwa mkurugenzi mtendaji mpya


MWANDISHI WETU Lagos, Nigeria

BENKI ya United ya Afrika Plc (UBA), imetangaza safu mpya ya uongozi huku Oliver Alawuba, akiteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa UBA Africa, anayesimamia shughuli za nchi 20 za Afrika ukitoa Nigeria.


Hatua hiyo inatokana na baadhi ya viongozi wake kustaafu katika bodi akiwamo Victor Osadolor, ambaye alitumikia nafasi hiyo kwa miaka tisa.


UBA for Africa inahudumia wateja zaidi ya milioni 19 katika Bara la Afrika, ikitoa huduma za rejareja, biashara na taasisi za kitaifa na inaongoza katika huduma jumuishi za kifedha na utekelezaji wa miradi katika nchi za Afrika.


Taarifa iliyotolewa na benki hiyo jana, ilieleza kuwa UBA inatajwa kuwa ni moja ya benki iliyowasiliana na mteja moja kwa moja kupitia chatbot iitwayo LEO.


Alawuba ana miongo mitatu ya uzoefu katika tasnia ya benki. Ambapo pia aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa UBA Ghana na baadaye kuwa Mkurugenzi Mtendaji UBA Africa kabla ya kurudi Nigeria kuendesha Benki ya UBA ya ukanda wa mashariki.


Chini ya uongozi wake, Benki ya UBA ya ukanda wa Mashariki imekuwa ni benki inayokua kwa kasi zaidi katika Afrika.


“Pia Bodi ilimteua msenegali, Abdoul-Aziz Dia kama Mkurugenzi Mtendaji wa Hazina na huduma ya benki Kimataifa, kwa idhini ya Benki Kuu ya Nigeria. Aziz anakuwa mkurugenzi mtendaji na atasaidia kwa zuoefu wake aliopitia nchi mbalimbali kukuza maendeleo ya benki ya UBA.


“Dia atawajibika kwa mtandao wa kimataifa wa shughuli za UBA huko New York, London na Paris, pamoja na Hazina kwa ujumla, ambapo UBA inatoa sehemu kubwa ya bidhaa kwa mataifa, taasisi za kimataifa na wateja wa Afrika,” ilieleza taarifa hiyo


Mbali na hao pia Chukwuma Nweke, ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa huduma za rejareja na malipo, ambapo ameonyesha dhamira yake kwenye taasisi kwa upande wa huduma za kibenki za rejareja.


Chukwuma ana karibu miongo mitatu ya uzoefu wa benki unaochukua Operesheni za Benki, Fedha, Teknolojia, ukaguzi na mkakati.
Bodi pia ilitangaza uteuzi wa Chiugo Ndubisi kama Mkurugenzi mkuu na mkuu wa uendeshaji wa UBA kwa idhini ya Benki Kuu ya Nigeria.


Akizungumzia kuhusu uteuzi huo, Mwenyekiti wa UBA, Tony O. Elumelu alisema “Miadi hii inasisitiza kujitolea kwa UBA kwa mtandao wetu wa Afrika na wa ulimwengu, msingi wetu mkubwa wa wateja na miundombinu yetu ya utendaji. Tunaangazia kuboresha ufanisi wetu na kuimarisha zaidi utumishi wetu kwa Afrika, kwa kutumia vipaji vya ajabu na uzoefu unaopatikana katika taasisi yetu,” alisema.


Elumelu amewashukuru Mkurugenzi Msaidizi / Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake wa uongozi wa UBA Afrika, Victor Osadolor na Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa UBA kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Emeke Iweriebor, ambaye amestaafu katika bodi, kwa michango yao mikubwa waliotoa kwa Benki ya UBA.


“Victor na Emeke walikuwa watu muhimu wakati wa kuunganishwa kwa Benki ya Standard Trust na UBA na wamekuwa wachangiaji muhimu katika ukuaji wa Benki. Tunawatakia maisha mema,” alisema Tony.


Uteuzi mpya wa Bodi umezingatia uwekezaji mkubwa katika rasilimali watu kwa kuchagua watendaji wenye sifa stahiki na utendaji mkubwa kaika kuendeleza benki.


Benki ya UBA imeweza kukaribisha wafanyakazi wapya 3000 kwa mwaka 2019, na kuwaongeza vyeo Zaidi ya wafanyakazi 5000. UBA ni muajiri mkubwa katika sekta ya benki Nigeria ikiwa na waajiriwa Zaidi ya 20,000 kwa grupu nzima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles