22.9 C
Dar es Salaam
Monday, September 9, 2024

Contact us: [email protected]

Benjamin Mkapa yadhamiria kupata ‘divison one’ 150

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa, Joseph Deo amesema kutokana na jitihada za walimu na wanafunzi mwaka huu wanatarajia kupata wanafunzi wenye ufaulu wa daraja la kwanza 150.

Shule hiyo ina wanafunzi 1531 wa kidato cha kwanza hadi sita na kati yao wanafunzi 128 ni wenye ulemavu.

Wanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa wakiimba wakati wa mahafali yao yaliyofanyika Dar es Salaam.

Akizungumza Oktoba 12,2023 wakati wa mahafali ya kidato cha nne amesema mwaka 2022 wanafunzi waliopata daraja la kwanza walikuwa 102 huku ufaulu ukiwa asilimia 99.

Amesema mwaka 2020 ufaulu ulikuwa asilimia 96, mwaka 2021 asilimia 97 wakati kwa kidato cha sita mwaka 2021 ulikuwa asilimia 100, mwaka 2022 asilimia 99 na mwaka 2023 asilimia 99.

“Mwaka huu tutafanya maajabu, tunaamini kwa jitihada za walimu na wanafunzi tutapunguza ‘division zero’ ikiwezekana kupata ‘division one’ 150 au zaidi…tunaweza,” amesema Deo.

Mkuu huyo wa shule amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutatua changamoto za shule hiyo ambapo ujenzi wa ukumbi, maktaba na uwanja kwa kuweka nyasi bandia unaendelea.

Naye Ofisa Elimu Taaluma Elimu Maalumu katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Pilly amesema Benjamin Mkapa ni miongoni mwa shule zinazofanya vizuri kitaaluma katika jiji hilo na kuwapongeza walimu kwa kazi nzuri.

“Deo (Mkuu wa shule) tangu akanyage Benjamin ametupaisha, analibeba Jiji la Dar es Salaam vizuri sana, walimu wanafanya kazi nzuri ndiyo maana wazazi wanakimbilia shule ya Benjamin,” amesema Pilly.

Mgeni rasmi katika mahafali hayo Mkurugenzi wa Zamaradi Media, Zamaradi Mketema, amejitolea kuwahudumia wanafunzi wawili wanaoishi kwenye mazingira magumu kwa kipindi chote mpaka watakapohitimu masomo yao.

Mkurugenzi wa Zamaradi Media, Zamaradi Mketema, akizungumza wakati wa mahafali ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa.

Wanafunzi hao ambao ni wa kidato cha kwanza mmoja ni yatima na mwingine ni kiziwi ambaye aliacha shule kutokana na kushindwa kumudu gharama za nauli, chakula na mahitaji mengine ya kibinadamu.

Zamaradi pia alichangia Sh 500,000 kwa kula keki iliyoandaliwa na wanafunzi wa shule hiyo kwa lengo la kuwasaidia wenzao wenye mazingira magumu kupitia mfuko maalumu waliouanzisha (Charity Group Foundation).

Katika mahafali hayo wanafunzi 254 walihitimu na baadhi yao walizawadiwa kwa kufanya vizuri katika maeneo mbalimbali.

Shule hiyo pia iliwazawadia walimu waliowezesha wanafunzi wa kidato cha sita mwaka 2023 kufanya vizuri ambapo ufaulu ulikuwa asilimia 99.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles