22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 18, 2021

BENITEZ AIREJESHA NEWCASTLE LIGI KUU

LONDON, ENGLAND


KOCHA wa klabu ya Newcastle United, Rafa Benitez, amefanikiwa kuirejesha timu hiyo katika michuano ya Ligi Kuu nchini England msimu ujao, baada ya kuichapa timu ya Preston kwa mabao 4-1.

Mshambuliaji wa Newcastle United, Ayoze Perez, alikuwa mwiba kwa wapinzani wao baada ya kufunga mabao mawili, huku mabao mengine yakifungwa na Christian Atsu pamoja na Matt Ritchie, huku bao la kufutia machozi la Preston likiwekwa wavuni na Jordan Hugill.

Benitez amewapa furaha mashabiki wa timu hiyo kwa kurudi tena kwenye mshike mshike wa Ligi Kuu msimu ujao, lakini kocha huyo baada ya kuipandisha daraja hajaweka wazi kama ataendelea kukifundisha kikosi hicho msimu ujao.

“Najua mashabiki wangu wamekuwa na sapoti kubwa hadi kuifanya timu hiyo kufuzu kushiriki Ligi Kuu msimu ujao, nimekuwa na furaha kwa kipindi chote kutokana na ushirikiano ambao nimekuwa nikiupata kutoka kwa wachezaji wa timu hii, ninaamini ushirikiano wao umetufanya tuwe hapa leo hii.

“Wengi walishangaa maamuzi yangu ya kuifundisha timu hii, lakini niliamua kufanya hivyo kwa ajili ya kusaidia ifike mbali na sasa ndoto zangu zimeanza kutimia na najivunia kwa kile ambacho ninakifanya.

“Huu ni muda sasa wa kufurahia kwa kile ambacho tulikuwa tunakipigania, kikubwa ambacho kimebaki kwa sasa ni kuhakikisha timu inafanya maandalizi ya kutosha ili kuweza kufanya makubwa katika michuano ya Ligi Kuu, kwa kuwa kuna ushindani wa hali ya juu,” alisema Benitez.

Hata hivyo, kocha huo amedai hana uhakika kama ataendelea kuwa kocha wa timu hiyo msimu ujao, mara baada ya kuipandisha daraja timu hiyo.

“Ni kweli najivunia kuwa hapa kwa sasa, kwa kuwa tayari nimepata mafanikio ambayo nilikuwa nayatafuta, lakini siwezi kujua kama nitaendelea kuwa hapa hadi msimu ujao, chochote kinaweza kutokea, ila sina uhakika kama nitakuwa kocha wa timu hii,” aliongeza.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,215FollowersFollow
521,000SubscribersSubscribe

Latest Articles