22 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

Bendi ya Waluguru yamkuna Super Nyamwela

Nyamwela 3NA FESTO POLEA, MOROGORO

BENDI ya Waluguru yenye maskani yake mkoani Morogoro, ilionyesha kumkuna mcheza dansi wa bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’, Super Nyamwela, baada ya kumpigia sebene kama alivyotaka.

Super Nyamwela alicheza vema sebene hilo na kujikuta akijizolea kiasi kikubwa cha fedha za kutunzwa na wapenzi wa muziki wa dansi waliofurika katika shindano la madansa wa zamani wa Morogoro na Dar waliokutana katika ukumbi wa Samaki Samaki mkoani Morogoro juzi.

Awali, Small Jobiso na Super Nyamwela, walialikwa katika kunogesha shindano hilo hivyo baada ya kuombwa kuonyesha chochote kama ishara ya salamu kwa mashabiki wa muziki wa dansi, Super Nyamwela aliomba bendi ya Waluguru inayotumbuiza katika ukumbi huo kila wikiendi impigie sebene la live nao wakafanya hivyo.

Bendi hiyo inazidi kujizolea mashabiki mkoani humo kutokana na uwezo wake mkubwa wa kupiga nyimbo za wasanii mbalimbali ‘copy’ kwa ufasaha huku wanenguaji wake wakionyesha umahiri mkubwa wa kucheza na kuimba nyimbo zao na za Kikongo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,284FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles