24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

Ben Pol: Nami nitamfurahia mwanangu kwa sherehe

Ben Pol
Ben Pol

IKIWA kama utamaduni kwa wasanii maarufu kuwafanyia sherehe kubwa watoto wao wanapotimiza miaka kadhaa ya kuzaliwa kwao mkali wa wimbo wa ‘Moyo Mashine’, Benard Paul ‘Ben Pol’, naye amesema lazima atafanya sherehe ya mwanaye akitimiza mwaka mmoja hata kama haitakuwa kubwa kama walizofanya wasanii wengine.

Ben Pol alisema miezi saba ijayo mtoto wake atatimiza mwaka mmoja na kwa kuwa ni wa kwanza lazima atamfanyia sherehe ikiwa ni kumshukuru Mungu kwa kumjalia mtoto huyo kutimiza mwaka.

“Sijapanga kufanya sherehe kubwa lakini akitimiza mwaka mmoja lazima nitamfanyia sherehe hata kama si kubwa lakini lazima nifanye sherehe kama shukrani kwa kutimiza mwaka na kuonyesha furaha yangu kupata mtoto,” alieleza.

Baadhi ya wasanii waliowahi kuwafanyia sherehe kubwa watoto wao walipotimiza miaka kadhaa ni pamoja na mkali wa Bongo Fleva nchini, Abdul Nassib ‘Diamond’ na mpenzi wake Zari, mwigizaji wa filamu, Anty Ezekiel na mpenzi wake mnenguaji wa Diamond, Iyobo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles