BEN POL KUFANYA ‘COLABO’ NA TREY SONGZ

0
864

NA JESSCA NANGAWE


MKALI wa muziki wa RnB nchini, Bernad Paul ‘Ben Pol’, anatarajia kufanya kazi na mkali wa muziki huo nchini Marekani, Trey Songz.

Mipango ya kufanya kazi pamoja imetokana na wimbo mpya wa Ben Pol, ambao unajulikana kwa jina la ‘Tatu’ aliomshirikisha Darasa, wimbo huo unaonekana kuvuka mipaka na kuongeza idadi kubwa ya mashabiki.

Ben Pol amesema anafurahi kuona wimbo wake huo ukipokelewa vizuri ndani na nje ya nchi, huku baadhi ya wasanii wakijitokeza kutaka kufanya naye kazi.

“Nina ‘collabo’ nyingi zinakuja kutoka kwa wasanii wa Nigeria, Marekani, ngoma yangu mpya ya Tatu imenifungulia njia, ninaamini bado nina nafasi ya kuendelea kuwa na mafanikio makubwa,” alisema Ben Pol.

Alisema miongoni mwa wasanii wa kimataifa anaotarajia kufanya nao kazi ni pamoja na Chidinma wa Nigeria na Trey Songz kutoka Marekani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here