30 C
Dar es Salaam
Friday, January 27, 2023

Contact us: [email protected]

BEN POL, BARAKA THE PRINCE WAMCHANGIA MWENZAO

Na MARY PETER–DAR ES SALAAM


WASANII watatu, Benald Paul (Ben Pol), Baraka the Prince na Juma Jux (Jux) wamechanga Sh 800,000 kwa ajili ya kumsaidia msanii mwenzao, Jet Man, anayehitaji fedha kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa maradhi yanayomsumbua yanayomsababishia asiweze kutembea.

Ben Pol alifafanua kwamba, baada ya onyesho lao la Love, Melody and Lights, katika fedha walizoingiza walitoa Sh 500,000 na pia wasanii hao walinunua biti iliyotengenezwa na Jet Man kwa kila mmoja kutoa Sh 100,000 kila mmoja, zikawa Sh 800,000 wakampelekea msanii huyo ili zimsaidie.

“Katika fedha tulizoingiza tumetoa Sh 500,000 na pia tumeongeza kila mmoja Sh 100,000, imefika Sh 800,000 tumempa rafiki yetu na msanii mwenzetu kwa mapenzi yetu ili zimsaidie katika baadhi ya mahitaji yake,’’ alisema Ben Pol. Ben Pol aliongeza kwamba, licha ya kusaidia kiasi hicho pia wasanii hao wakishirikiana na mchekeshaji Mc Pilipili wameandaa tamasha mkoani Dodoma ambalo pia watatenga kiasi cha fedha kwa ajili ya kumchangia msanii huyo mwenye uhitaji mkubwa wa fedha kwa ajili ya kufanyiwa tiba ya matatizo yanayomsumbua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles