28.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Ben Pol awang’ata sikio wanaume kuhusu pete za wapenzi wao

Beatrice Kaiza

BERNARD PAULO a.k.a Ben Pol ni miongoni mwa majina makubwa kwenye tasnia ya muziki hapa Bongo sababu ya mengi aliyoyafanya na kufanikiwa kujitengenezea mashabiki Afrika Mashariki na Kati.

Miaka yake 10 kwenye muziki, imekuja na mabadiliko mengi yaliyomfanya aendelee kuwa Ben Pol mpya kila leo huku akitoa nyimbo zinazopokewa vizuri na mashabiki zake.

Katikati ya  wiki, Ben Pol alifika kwenye ofisi za gazeti hili na kupiga stori kadhaa na Swaggaz kuhusu maisha na muziki wake ikiwa ni siku chache baada ya kuachia wimbo, Ebenezer.

Swaggaz: Sababu gani zimefanya uje na wimbo wa Injili?

Ben Pol: Kadri Mungu anavyonijalia uhai na pumzi nitakuwa namwimbia yeye na ukuu wake katika mambo anayowatendea wanadamu na faida za kumwamini, kwahiyo nyimbo kama hizo zitaendelea kuwepo tu ila siyo sijaingia moja kwa moja kwenye gospo.

Swaggaz: Ebenezer ilitengenezwa vipi studio?

Ben Pol: Tukiwa studio mimi na prodyuza Tidy Hotter hiyo vibe ilikuja ikawa inatupeleka kwenye gospo hasa ukizingatia nilikuwa na nia ya muda mrefu ya kufanya wimbo wa Mungu, nikasema huu ndiyo muda sahihi, nikaangalia ushuhuda wangu na vile Mungu amenipitisha ndiyo Ebenezer ikazaliwa.

Swaggaz: Ni kweli muziki wa Tanzania umemezwa na ladha kutoka Nigeria?

Ben Pol: Ni kweli, watu wengi wanashindwa kubuni, ‘sampling’ nyingi sana, watu wanachukua vionjo vya kinigeria, watu wanaona uvivu kuwachambua kina Mbaraka Mwishehe kina Marijani Rajab, kuna madini mengi sana huko kwa kina Sikinde, Msondo, huko ndiyo kuna utambulisho wetu, mtu anaenda studio na mdundo wa Davido anamwambia prodyuza hebu tupite humu, nadhani watu inatakiwa tuchimbue.

Swaggaz: Ukiacha muziki, ni kweli ulimvisha pete ya uchumba mpenzi wako Anerlisa yenye thamani ya milioni 20?

Ben Pol: Ni upendo tu, mimi nataka niwape ushauri wanaume wenzangu ambao sasa wanataka kuingia kwenye mapenzi au wako kwenye mapenzi. Mpenzi wako anaweza kukupima kulingana na pete uliyomchukulia iwe ya uchumba au ndoa.

Pale anaanza kuangalia ‘usiriazi’ wako kwahiyo kama una uwezo na mpambanaji, pambana umtafutie mpenzi wako pete nzuri ambayo hata mwenyewe akikaa peke yake anajisikia vizuri kiasi kwamba anaweza kwenda sokoni kidole kipo juu, mfanye ajisikie umepambana, mimi niliona hicho kitu ninaweza kukifanya na kama mtu unampenda kwanini ushindwe.

Swaggaz: Umekaa kwenye muziki kwa miaka 10 sawa na Diamond Platnumz, yeye alifanya jambo kule Kigoma wewe kuna namna yoyote utasherehekea?

Ben Pol: Kuna mengi sana nimepanga kufanya mwaka huu kama sehemu ya kushukuru kwa miaka 10 kwenye muziki na vitakuwa vinaenda kwa mpangilio, mwezi Aprili kuna tukio, Juni kuna tukio, Septemba pia kuna tukio na Desemba kuna tukio na yote yatahusu miaka yangu 10 kwenye muziki.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles