21.1 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Bemba hatiani kwa kuhonga mashahidi

Jean-Pierre Bemba
Jean-Pierre Bemba

THE HAGUE, Uholanzi

MAHAKAMA ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imemkuta na hatia aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Jean-Pierre Bemba ya kuhonga mashahidi.

Mapema mwaka 2016, Bemba alipatikana na hatia ya kutekeleza uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu na alihukumiwa kifungo cha miaka 18 gerezani.

Lakini pia juzi alipatikana na kosa la kuwahonga mashahidi na kuvuruga ushahidi katika kesi hiyo.

Washirika wake wanne wa karibu pia walipatikana na makosa sawa na hayo.

Kesi hiyo ni ya kwanza ya ufisadi kuendeshwa katika mahakama hiyo iliyoko jijini hapa.

Mahakama hiyo iliambiwa kuwa Bemba alishiriki njama ya kuwahonga mashahidi akiwa gerezani wakati kesi yake ya kwanza ilipokuwa ikiendelea.

Washirika wake walitumia simu za siri na lugha za mafumbo kuwahonga, kuwafunza na kuwaelekeza mashahidi 14 walioitwa kutoa ushahidi katika kesi hiyo.

Kesi hiyo ililetwa mahakamani baada ya ofisi ya mwendesha mashtaka kupashwa habari kuhusu maovu hayo.

“Akitoa hukumu hiyo, Jaji Bertram Schmitt alisema kesi hiyo “ilikuwa ya wazi na washukiwa hao walijaribu kuvuruga mfumo wa haki, jambo ambalo ni kosa kubwa sana”.

Machi mwaka huu, Bemba alihukumiwa kwa makosa aliyoyatekeleza katika taifa jirani la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Afrika Kati (CAR) mwaka 2002 hadi 2003.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,592FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles