27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

BEKI WA REAL MADRID AVUNJIKA MBAVU

MADRID, HISPANIA


BEKI kisiki wa mabingwa watetezi wa Klabu Bingwa barani Ulaya, Real Madrid, Kepler Ferreira, maarufu kwa jina la Pepe, ataikosa michezo ya robo fainali Ligi ya Mabingwa baada ya kuvunjika mbavu kwenye mchezo wa Ligi Kuu nchini Hispania juzi.

Mchezaji huyo amevunjika mbavu mbili baada ya kugongana na mchezaji mwenzake wa timu hiyo, Toni Kroos, wakati wa mchezo dhidi ya wapinzani wao Atletico Madrid, huku mchezo huo ukimalizika kwa sare ya 1-1.

Baada ya kuumia mchezaji huyo alikimbizwa hospitalini kufanyiwa vipimo na kugundulika kuwa mbavu mbili zimevunjika, hivyo atakuwa nje ya uwanja na kuikosa michezo yote miwili ya robo fainali dhidi ya Bayern Munich.

Real Madrid wanatarajia kukutana na wapinzani wao Bayern Munich keshokutwa katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya kwanza Ligi ya Mabingwa Ulaya, hivyo watakuwa na wakati mgumu kumkosa mchezaji huyo katika michezo hiyo muhimu.

“Daktari katika Hospitali ya Sanitas La Moraleja University, amegundua kuwa Pepe amevunjika mbavu mbili pamoja na kupata misuguano kwenye mbavu nane za upande wa kushoto,” waliandika kwenye mtandao wa Madrid.

Kocha wa klabu hiyo, Zinedine Zidane, ameweka wazi kuwa kikosi chake kitakuwa katika wakati mgumu kumkosa mchezaji huyo ambaye amekuwa imara katika safu ya ulinzi akishirikiana na Sergio Ramos.

“Pepe ni miongoni mwa wachezaji wenye uwezo mkubwa katika safu ya ulinzi, taarifa iliopo ni kwamba amepata tatizo kwenye mbavu hivyo tutamkosa katika mchezo dhidi ya Bayern Munich Jumatano, ambao ni wa kwanza wa robo fainali.

“Sina uhakika kama ataweza kuwa fiti kwa mchezo ujao wa marudiano, lakini tuna kikosi kipana ambacho kinaweza kufanya makubwa zaidi katika michezo hiyo,” alisema Zidane.

Hata hivyo, nafasi ya Pepe ilidaiwa kutaka kuchukuliwa na beki wao, Raphael Varane, lakini inasemekana kuwa anaweza kuwa nje ya uwanja kutokana na kusumbuliwa na matatizo ya nyama za paja. Kutokana na hali hiyo, Zidane atalazimika kumtumia Ramos na Nacho katika safu ya ulinzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles