30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, March 26, 2023

Contact us: [email protected]

Beki mpya awapigia saluti mashabiki Yanga

Theresia Gasper -Dar es salaam

BEKI mpya wa Yanga raia wa Burundi, Mustafa Seleman, amesema katika maisha yake ya soka hajawahi kucheza timu yenye idadi kubwa ya mashabiki Yanga.

Seleman ametoa kauli hiyo baada ya kushuhudia mashabiki wa Yanga wakiwa wameujaza uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati wa mechi ya kilele cha Wiki ya Mwananchi dhidi ya Kariobang Sharks.

Katika mchezo huo ambao walitoka sare ya bao 1-1,  ulikuwa wa utambulisho kwa wachezaji wapya na Seleman ni mmoja wa nyota walioonyesha kiwango kizuri na kuwafanya Wanajangwani hao kushangilia muda mwingi.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Seleman alisema, alishangazwa na umati mkubwa wa mashabiki waliojitokeza uwanjani kuisapoti timu yao.

“Hii ni mara yangu ya kwanza kucheza timu ambayo ina mashabiki wengi kama ilivyokuwa Yanga, kwani walijitokeza kwa wingi hali iliyonipa morali ya kucheza kwa kujituma zaidi,” alisema.

Alisema licha ya kupata matokeo ya sare wataendelea kujituma ili kuwapa furaha mashabiki wao na kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa inayowakabili na Ligi Kuu Tanzania Bara.

Seleman aliwataka mashabiki waendelee kuwapa sapoti katika mechi zao kwani hali hiyo itazidi kuwapa morali ya juu zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,195FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles