BEKA KUZINDUA BENDI YAKE APRILI 29

0
624

Na GLORY MLAY


MSANII wa Bongo Fleva, Beka Ibrozoma, anatarajia kuzindua bendi yake aliyoipa jina la ‘Spidoch Band’ kwenye ukumbi wa Club Next Door uliopo jijini Dar es Salaam.

Uzinduzi huo utakaofanyika Aprili 29 mwaka huu, unatarajiwa kuleta hamasa kwa wasanii wengine kuwekeza katika bendi ili wawe na wigo mpana wa kupiga muziki wa mubashara.

“Mashabiki ndio kila kitu, nawaomba wajitokeze kwa wingi ili nifanikishe uzinduzi wa bendi yangu iweze kufanya kazi kihalali kwa kulipa kodi, nami pia nipate kipato cha kukidhi matakwa yangu lakini pia tutanue wigo wa muziki wetu,” alisema Beka. 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here