25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

BEI ZA VYAKULA NCHINI ZAPAA

Na VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

MFUMUKO wa bei za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Februari, mwaka huu, umeongezeka hadi asilimia 8.7 kutoka asilimia 7.6, Januari mwaka huu.

Kaimu Meneja, Idara ya Ajira na Bei wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ruth Minja, alisema hayo jana Dar es Salaam alipokuwa akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari.

Alisema mfumuko wa bei wa taifa mwezi Februari, mwaka huu umeongezeka hadi kufikia asilimia 5.5 kutoka asilimia 5.2 ya Januari, mwaka huu.

“Hii inamaanisha kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Februari, mwaka huu, imeongezeka ikilinganishwa na kasi ya upandaji wa bei ilivyokuwa kwa mwezi ulioishia Januari, mwaka huu.

“Kuongezeka kwa mfumuko wa bei Februari mwaka huu, kumechangiwa hasa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula kwa kipindi kilichoishia Februari, mwaka huu zikilinganishwa na bei za mwezi Februari, mwaka jana.

“Mfumuko huo wa bei kwa Februari, mwaka huu, unapimwa kwa kipimo cha mwezi, umeongezeka kwa asilimia moja ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 0.8 ilivyokuwa Januari, mwaka huu.

“Mfumuko huo wa bei umezigusa bidhaa kama mchele uliopanda kwa asilimia nne, mahindi kwa asilimia 12.2, unga wa mahindi kwa asilimia 10.1, mtama kwa asilimia 5.6, ndizi za kupika kwa asilimia 9.5 na maharage kwa asilimia 6.7,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles