27.6 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Bei ya vifaa vya shule yapanda maradufu Kariakoo

Aveline Kitomary, Dar es salaam 

Baadhi  ya wazazi wamelalamikia kupanda kwa bei ya vifaa vya shule katika soko la Kariakoo  jijini Dar es salaam kuelekea kipindi hiki cha  kufunguliwa kwa shule.

Akizungumza  na Mtanzania Digital kwa leo Jumatatu Desemba 31,  mmoja wa wazazi hao Mariam Salmin amesema awali vifaa hivyo vilikua vinauzwa kwa bei ya chini lakini kipindi hiki cha kueleka kufunguliwa kwa shule bei zimepanda mara mbili.

Mariam amesema wanawaomba wafanyabiashara wapunguze bei ya vifaa na wauze kama walivyokuwa wanauza mwazo.

“Nimeulizia bei ya shati hapa wameniambia ni Sh. 12,000  nimeshindwa hata kununua, hapa naenda  kuongeza hela nirudi tena kununu,”amesema Mariam.

Bei ya vifaa imepanda ambapo shati la shule aina  ya ‘Tomato’ ilikuwa inauzwa kuanzia Sh. 6,000 hadi 8,000 kwa sasa linauzwa kuanzia Sh. 10,000 hadi 12,000, bei ya viatu ilikuwa Sh.  5000 hadi 10000 sasa wanauza shilingi 15,000 hadi 30,000 huku bei ya madaftari makubwa aina ya ‘Counter book’ ilikuwa inauzwa Sh. 2,000 kwa sasa linauzwa Sh  3,000.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,186FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles