27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Bei ya mafuta yashuka maradufu

Petrol_pump_mp3h0354Na Mwandishi Wetu

-DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati na Maji na Mafuta (Ewura), imetangaza kushuka bei ya mafuta ya aina zote kwa jumla na rejareja.

Bei hizo mpya ya mafuta zimeshuka katika mikoa yote isipokuwa Mkoa wa Tanga, hasa kwa petroli, dizeli na mafuta ya taa.

Taarifa ya Ewura jana ilisema bei hizo zimeshuka ikilinganishwa na toleo la bei za mafuta hayo lililopita la Agosti 3, mwaka huu.

Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Felix Ngamlagosi, alisema katika toleo hilo, bei ya rejareja kwa petroli, dizeli na mafuta ya taa imepungua kwa viwango tofauti.

Alisema kwa petroli imeshuka kwa Sh 65, dizeli Sh 63 na mafuta ya taa Sh 86.

“Bei ya jumla imepungua ambako kwa petroli ni Sh 65.31, dizeli Sh 63.39 na mafuta ya taa Sh 85.93,” alisema.

Ngamlagosi alisema kushuka kwa bei ya petroli katika soko la dunia na kupungua kwa gharama za usafarishaji/uletaji wa   mafuta hayo nchini, ndizo sababu kuu zilizochangia  kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la ndani nchini.

“Bei ya jumla na rejareja kwa petroli na dizeli katika Mkoa wa Tanga imeongezeka kidogo ikilinganishwa na toleo la bei za mafuta hayo lililopita la Agosti 3, 2016.

“Katika toleo hili, bei ya rejareja kwa petroli na dizeli imeongezeka kwa viwango ambavyo petroli ni Sh 50 na  dizeli Sh 19. Kwa kulinganisha na matoleo haya mawili, bei ya jumla imeongezeka.

“Petroli Sh 49.61 kwa lita sawa na asilimia 2.80 na dizeli Sh 18.57 kwa lita sawa na asilimia 1.1.

“Ongezeko hili la bei limechangiwa kwa kiasi kikubwa na kupokea mafuta mapya (petroli na dizeli) ndani ya Agosti 2016, ambayo yalitarajiwa kupokewa Julai 2016 na pia kutokupokea mafuta mapya kutoka  katika meli ya MT. Nevaska Lady ndani ya Agosti mwaka huu,” alisema Ngamlagosi.

Hata hivyo, alisema mamlaka hiyo inawakumbusha wananchi kwamba bei kikomo ya mafuta kwa eneo husika, pia inapatikana kupitia simu zao za mkononi kwa kupiga namba *152*00# na kufuata maelekezo.

Alisema huduma hiyo hutolewa bure na inapatikana kupitia mitandao yote ya simu za mkononi nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles