27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Bayport yakabidhi bodaboda kwa mtumishi wa Muhimbili

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

TAASISI ya kifedha ya Bayport Financial Services, imekabidhi bodaboda mpya aina ya Hunter kwa mtumishi wa Hospital ya Taifa Muhimbili, Robert Lukanga, aliyoshinda katika promosheni ya taasisi hiyo iliyozinduliwa mapema mwezi huu ambapo kila mwezi watapatikana washindi wawili waliokopa fedha na kupata tiketi ya kushinda pikipiki hizo za kisasa.

Akizungumza leo Alhamisi Novemba 18, katika makabidhiano hayo nje ya jengo la dharula kwenye hospital hiyo ya Taifa Muhimbili, Lukanga alisema amejisikia furaha kuwa mtu wa kwanza kushinda bodaboda kutoka Bayport, akiamini itasaidia katika harakati zake za kimaisha za kila siku.

Amesema awali lengo lake lilikuwa ni kukopa fedha za Bayport ili zisaidie katika kuinua kiwango chake cha uchumi, hivyo kujulishwa juu ya ushindi wake wa bodaboda umekuja wakati muafaka kwa kuwa chagizo la kuboresha kipato chake cha kila siku.

“Kwakweli sikutarajia kama ningeweza kupigiwa simu kuelezwa juu ya ushindi wangu wa pikipiki aina ya Hunter kutoka kwenye taasisi hii ambayo siku zote imekuwa tegemeo kwetu sote watumishi wa umma.

“Naomba Watanzania wote tukope Bayport ili tujiweke katika nafasi nzuri za kushinda boboda ambapo kila mwezi washindi wawili watakuwa wamepatikana, ambapo mimi nilitangazwa katika droo ya Novemba 15, huku Novemba 30 pia akitafutwa mshindi mwingine,” amesema.

Naye Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, amesema kila anayekopa kwenye taasisi yao anaingia kwenye droo moja kwa moja kwa ajili ya kushinda bodaboda, ambapo wote wanaweza kukopa kwa kupitia viganja vyao kwa kupiga namba 0800782700.

“Kama wewe ni mtumishi wa umma unaweza kukopa kwa kupiga simu badala ya kutembelea ofisini kwetu, huku pia mfumo wetu wa ukopaji ukiwa ni rahisi na unaotoa huduma nzuri tukiamini tutakuwa chachu ya ukuzaji wa uchumi wa Watanzania wote,” amesema Cheyo.

Bayport ni taasisi inayoongoza kutoa mikopo kwa watumishi wa umma kwa njia rahisi na nyepesi, ambapo katika makabidhiano hayo ya bodaboda kwa mtumishi wa Muhimbili huku Abdallah Kiwanga, akimwakilisha Afisa Utumishi wa Muhimbili katika tukio hilo la kukabidhiwa bodaboda kwa Lukanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles