BAYERN Munich hawana mpango wa kumsajili beki wa Kijerumani anayekipiga Chelsea, Antonio Rudiger.
Aliyekana tetesi hizo zilizosambaa ni mkurugenzi wa michezo wa Bayern, Hasan Salihamidzic.
Licha ya kukiri si vizuri kuzungumzia mchezaji wa klabu nyingine, Salihamidzic amesema Bayern haina udhaifu kwenye eneo la beki wa kati.
“Tumejiimarisha vizuri kwa kusajili wachezaji wakubwa kama Dayot Upamecano na pia tuna Lucas Hernandez, Tanguy Nianzou na Benjamin Pavard anayeweza kucheza pia nafasi ya beki, tumejitosheleza kabisa,” amesisitiza.