30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 19, 2021

Bayern Munich wawaomba radhi Man City

MUNICH, UJERUMANI

MABINGWA wa Ligi Kuu nchini Ujerumani, Bayern Munich, wamewaomba radhi Manchester City baada ya kuvujisha picha za Leroy Sane mapema akisaini mkataba wa kuitumikia timu hiyo.

Picha hizo zilipostiwa Alhamisi kwenye website wa Bayern Munich na baada ya muda kuenea kwenye kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii.

Kutokana na hali hiyo uongozi wa timu ya Bayern Munich umewaomba radhi viongozi wa timu hiyo kwa kuvujisha picha hizo mapema.

Inasemekana kuwa, mchezaji huyo amefikia makubaliano ya kujiunga na Bayern Munich akitokea Manchester City kwa uhamisho wa pauni milioni 55, lakini bado dili hilo halijakamilika kwa asilimia 100 baina ya pande zote mbili.

Mapema wiki iliopita kulikuwa na

taarifa kwamba, mchezaji huyo amefikia makubalianonatimuhiyokwamkataba wa miaka mitano baada ya kuweka wazi

hatima yake ndani ya Manchester City. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, msimu uliopita alikuwa na

thamani ya pauni milioni 130, lakini kwa sasa thamani hiyo imeshuka kutokana na janga la virusi vya corona, hivyo klabu nyingi zimeyumba kiuchumi.

Sane anakwenda kujiunga na Bayern Munich chini ya kocha Hans- Dieter Flick na atakuwa anachukua kitita cha pauni 350,000 kwa wiki, lakini hatokuwa kwenye kikosi kwa sasa hadi msimu ujao.

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, aliweka wazi kuwa, mchezaji huyo ataondoka wakati huu wa kiangazi, lakini hawana mpango wa kumsajili mchezaji wa kuziba nafasi yake kwa kuwa tayari yupo Phil Foden ambaye anaweza kucheza nafasi hiyo.

Mbali na Foden, kuna wachezaji wengine kama vile Riyad Mahrez na Raheem Sterling ambao wanaweza kucheza kwenye nafasi hiyo. Tatizo kubwa waliyokuwa nayo Manchester City ni safu ya ulinzi na sio kiungo wala ushambuliaji.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,848FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles