24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

BAVICHA YALAANI KUKAMATWA MEYA UBUNGO

Na ASHA BANI-DAR ES SALAAM

BARAZA la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha),  limelaani hatua ya wakuu wa wilaya na mikoa kuendeleza kutumia madaraka yao vibaya kwa kuwakamata viongozi mbalimbali hasa wa vyama vya upinzani.

Baraza hilo limesema hawafikirii kama Rais Dk. John Magufuli, anawatuma kuwakamata na kuwanyanyasa viongozi wa upinzani ambao wameshika nyadhifa mbalimbali ya kulitumikia taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bavicha, Patrobas Katambi alisema juzi Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob,  alikamatwa kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori, kwa kosa ambalo halina msingi zaidi ya udhalilishaji.

“Kukamatwa kwa Meya Jacob tunaambiwa sababu ni kutembelewa na aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu wa serikali ya awamu ya tatu Frederick Sumaye  kwa kudai kuwa walikuwa wakifanya mkutano  na kisha mkuu huyo kuagiza kukamatwa kwa Sumaye jambo ambalo ni kosa kwa kuwa hana mamlaka hayo,’’ alisema Katambi.

Alisema kuwa kinachofanyika kwa sasa ni uvunjifu wa sheria na suala hilo kuonekana kuwa linafanyika kisiasa.

Hata hivyo walishangazwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi, wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole  kuzunguka nchi nzima na kufanya vikao vya ndani lakini suala hilo limekuwa likizuiwa kwa wapinzani.

Katika hatua nyingine  amesema baraza hilo litakuwa la mwisho kumpongeza Rais Dk. John Magufuli katika sakata la kampuni ya kufua umeme ya IPTL, hadi hapo wahusika wakuu watakapokamatwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles