Bavicha Temeke yaunga mkono Chadema kutoshiriki uchaguzi

0
885

Elizabeth Joachim, Dar es Salaam

Bazara la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha) Wilaya ya Temeke, limesema linaunga mkono kauli ya Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, ya kutoshiriki chaguzi ndogo za marudio kutokana  na chaguzi hizo kutofanyika kwa haki.

Akizungumza na wandishi wa habari leo Jumamosi Septemba 29, jijini Dar es Salaam Katibu wa chama hicho, Benitho Mwapinga, amesema kwa sasa hawako tayari kushiriki chaguzi hizo hadi kufikia chaguzi za ambazo ni Serikali za Mitaa mwaka 2019 na Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.

Amesema chama hicho kipo imara na kwamba hakiwezi kutetereka licha ya baadhi ya viongozi na wanachama wake kuendelea kukihama chama hicho na kujiunga na  Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Naye Mwenyekiti Bavicha, Charles Gahu, ameutaka Umoja wa Vijana CCM (UVCCM), kuheshimu na kutambua mipaka yao dhidi ya chama chao na kutokumvunjia heshima Mwenyekiti wa chama chao.

“Tunaomba sana UVCCM waheshimu mipaka wana nguvu gani ya kuweza kujibizana na mwenyekiti wetu wa Taifa (Freeman Mbowe),  sisi hatuwezi kutoa kauli na kuanza kumjibu mwenyekiti wao tunaomba sana waheshimu mipaka” amesema Gahu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here