Batuli: Kama sio ‘Fake Smile’ ningekuwa rubani

0
1676

GLORY MLAY

MSANII wa filamu nchini, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ amesema kama sio filamu ya Fake Smile angekuwa rubani kwa sasa.

Batuli alikuwa na mpango wa kwenda kusomea urubani lakini kutokana na ushawishi aliopata kutoka kwa marehem Steven Kanumba akaamua kuingia kwenye uigizaji.

“Nilikuwa na mipango kabisa kwenda kusomea urubani lakini kuna siku nilikutana na Kanumba akaniambia kuwa naweza kuigiza kwasababu ameona ninakipaji, aliniambia kuwa anafilamu yake ya Fake Smile anataka kutoa kwa hiyo niende nikaigize.

“Nilienda lakini nilikuwa sijiamini kama naweza lakini walinipa moyo na tulifanya vizuri na pia kwenye mauzo sokoni yalikwenda vyema, basi kuanzia hapo wakaniambi wewe ni muigizaji hivyo kama nilikuwa na mipango mingine niache,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here