30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

BATULI AWATOLEA POVU WANAOMJADILI

Na SHARIFA MMASI


MWIGIZAJI mahiri wa filamu nchini, Youbnish Yusuph ‘Batuli’, amewataka mastaa wenzake kuacha kumjadili baada ya kuchukua maamuzi ya kutoa elimu ya dini kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Batuli alisema baada ya kuingia kwa mwezi Mtukufu wa Ramadhani, aliamua kutoa elimu kwa mashabiki wake lakini anashangazwa na baadhi ya watu wanaomjadili na kuwataka waache mara moja.

“Tangu kuanza kwa mwezi Mtukufu wa Ramadhani, niliamua kujitoa kwa ajili ya Allah kwa kuwapa mashabiki wangu elimu ya dini tofauti.

“Katika jambo lolote zuri, wabaya hawakosekani naamini wapo wanaoniona najifanyisha, lakini ukweli ni kwamba elimu hiyo ina manufaa kwa kila mmoja katika maisha ya duniani na akhera,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,896FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles