22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 14, 2024

Contact us: [email protected]

Basilla acharuka Korongwe

Na Jerenia Ernest, Mtanzania Digital

MKUU wa Wilaya ya Korogwe, Basilla Mwanukuzi, ameagiza kukamatwa na kuwekwa ndani kwa wakuu wa idara mbili ambao ni Mwenyekiti wa Kamati ya manunuzi Idara ya mipango na takwimu Yasin Msangi na  mkuu wa Idara ya manunuzi ambaye ni katibu wa kamati hiyo, Gregory Matandiko.

Agizo hilo linatokana na wakuu wa idara hizo kutuhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za serikali na kukiuka taratibu za manunuzi katika miradi.

Basilla ametoa uamuzi huo wakati wa ziara aliyofanya Jumatano Agost 25, akiambatana na kamati ya usalama ya wilaya katika miradi ya ujenzi wa jengo la utawala na Hospitali ya Wilaya Makuyuni.

Akizungumza na Mtanzania Digital, Basilla amesema katika ziara hiyo hakuridhishwa na ujenzi wa wodi tatu unaofanyika katika eneo hilo na usimamizi wa miradi mingine hivyo baada ya kukaa kikao cha ndani na kamati ya usalama wilaya, kamati zote za ujenzi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Korogwe, wakafikia uwamuzi wa kuwakamata wakuu wa idara hizo.

“Katika ziara niliyofanya nimegundua changamoto zinazosababisha kukwamisha miradi kutokamilika ni baadhi ya watendaji , nimeagiza kukamatwa kwa wakuu wa idara husika pia nimemwagiza Mkurugenzi wa Wilaya kuvunja kamati zote na kuteua wajumbe wapya katika idara hizo,” anasema Basilla.

Katika hatua nyingine ameagiza kusimama kwa shughuli zote za ujenzi wa miradi hiyo kwa kipindi cha siku 14 ili kujiridhisha na matumizi ya fedha zilizotumika hadi sasa katika miradi hiyo.

Aidha Basilla  amemwagiza Kamanda wa Takukuru, kuanza kufanya uchunguzi wa suala hilo kunusuru fedha za serikali zinazoibiwa na baadhi ya watumishi wasio waaminifu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles