20.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 28, 2022

BASHIRU AZUA GUMZO NDANI, NJE, CCM

Na ELIZABETH HOMBO-DAR ES SALAAM


SIKU moja baada ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kumteua Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Bashiru Ally, kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho tawala, wanazuoni na makada wakongwe wa chama hicho wametoa maoni yao.

Uteuzi wa Dk. Bashiru umekuja baada ya Mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli, kuridhia barua ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana mbele ya kikao cha NEC.

Halmashauri Kuu ambayo ni chombo cha juu kwa maamuzi ya juu ndani ya CCM, iliyokutana kwa siku mbili Ikulu Dar es Salaam, ilimpitisha msomi huyo aliyeongoza kamati iliyohakiki mali za chama hicho kwa miezi mitano.

Akizungumzia uteuzi huo wa Dk. Bashiru, Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala wa Umma UDSM, Dk. Rasul Minja, alisema wameupokea kwa furaha na fahari kwa chuo chao.

“Hii ni fahari kwetu, kwamba mwenzetu amepewa dhamana kubwa ndani ya chama tawala, ambacho kina historia kubwa Afrika.

“Bashiru si mtu wa kwanza kuteuliwa kufanya kazi katika taasisi ya Serikali, lakini kwetu ni wa kwanza mtu kama yeye kuteuliwa katika nafasi kubwa namna hiyo.

“Anakwenda kuvaa viatu vya Kinana, kazi aliyokuwa amepewa ya kuchunguza mali za CCM ilikuwa nzito, naona wameridhika na kamati yake, hivyo anaweza akasimamia. Hii kwetu ni furaha na faraja.

“Bashiru namfahamu si tu kama mfanyakazi mwenzetu, lakini tangu tukiwa wanafunzi tulisoma wote ‘degree’ (shahada) ya kwanza na ya pili, ni miongoni mwa waliofanya vizuri sana katika hatua zote hizo.

“Alionyesha dalili za uongozi tangu ‘degree’ ya kwanza,   tulikuwa naye katika kampeni ya kugombea uongozi wa Serikali ya Wanafunzi (DARUSO), lakini bahati mbaya hakupata.

“Ni mtu ambaye anaamini na kusimamia kile anachokizungumza, misimamo yake huwa haiyumbi, ni mzungumzaji mzuri,” alisema Dk. Minja.

Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,097FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles