30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Bashe: Wakulima jiungeni bima ya afya

Grace Shitundu – Simiyu

NAIBU Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, amewataka wakulima nchini kutumia fursa ya kujiunga na bima ya afya inayotolewa na Shirika la Bima ya Afya la Taifa (NHIF) ili kupunguza gharama za matibabu katika kaya.

Akizungumza na MTANZANIA Jumapili baada ya kutembelea banda la NHIF katika maonyesho ya Nanenane Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu, Bashe alisema bima hiyo itawapunguzia gharama ya matibabu.

Alisema kwamba bima hiyo inayokatwa kwa Sh 70,000 inaweza kukatwa na mkulima yeyote.

“Bima hii kila mwananchi atalipa Sh 70,000 ambayo itamsaidia yeye na familia yake watahudumiwa kwa pamoja.

“Bima itampunguzia gharama za matibabu kwa sababu gharama za matibabu ni kubwa sana katika kaya, na kaya zetu za kiafrika nyingi unakuta pamoja na baba na mama huwa kunakuwa na wengi.

Alisema kwa hiyo ni vizuri wakulima kutumia fursa hiyo kwenda ofisi za NHIF zilizopo kwenye mkoa, wilaya na kanda kupitia ushirika wao.

“Vyama vya ushirika ndio vyenye dhamana ya kwenda kuwajazisha fomu wenzao, kwa hiyo niwaombe wote washirikiane kuiunga mkono NHIF, hii itatusaidia sana kupunguza sana gharama za matibabu katika ngazi ya familia,” alisema Bashe.  

Aidha, Bashe amewapongeza NHIF kwa kuja na mfumo wa bima ya afya kwenye vikundi vya wakulima inayoitwa jina la Ushirika Afya.

“Ningependa kutumia nafasi hii kuwaomba wakulima ambao wapo kwenye Amcos waweze kutumia nafasi hii na kuweza kuitumia,” alisema Bashe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles