27.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Bashe: umaskini chanzo wakulima kuuza kahawa mbichi

Nyemo Malecela, Kagera

Naibu Waziri wa Kilimo na Ushirika, Hussein Bashe amesema umasikini ndiyo unasababisha wakulima wa kahawa mkoani Kagera wauze kahawa mbichi zikiwa bado shambani (butura).

Bashe amesema hayo jana wakati akizungumza na viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika mkoani Kagera ambapo ameviagiza vyama vya ushirika kuanzia msimu huu wa kahawa unaoanza Mei mwaka huu kutenga shilingi 30 kwa kila kilo kwa Chama cha Ushirika (Amcos).

Bashe alisema Chama Kikuu cha Ushirika (KDCU), kinatakiwa kutenga takribani Sh milioni 900 na Chama cha Ushirika cha Kagera (KCU) wanatakiwa kutenga kiasi hicho cha fedha ili kuondoa umasikini wa wakulima wa kahawa unaopelekea kuuza butura.

“Fedha hizo ziwekwe katika mfuko maalumu zirudi kwenye vyama vya msingi ili wakulima wawe wanakwenda kukopa kwa ajili ya mahitaji yao madogo badala ya kuuza kahawa yao ikiwa bado shambani,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, Bashe amewataka wananchi kutambua kuwa Kiwanda cha Kahawa cha TANICA kilichopo Manispaa ya Bukoba kuwa ni mali yao.

“Hivyo tumekubaliana na vyama vya ushirika na wananchi kuwa ili TANICA iweze kufanya kazi inahitaji takribani tani 1,500 ya kahawa safi na tani 3,000 ya kahawa yenye maganda.

“Tumekubaliana KDCU itatoa tani 1,200 na KCU itatoa tani 300 za kahawa ambazo zitaenda kuchakatwa katika kiwanda cha kahawa cha TANICA,” amesema.

Aidha, Bashe amesema haiwezekani kiwanda hicho kikose malighafi wakati vyama hivyo vya ushirika vina hisa katika kiwanda hicho.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,530FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles