31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Bashe: serikali imeimarisha utawala bora kukabiliana na viongozi wabadhirifu AMCOS

Mwandishi Wetu, Dodoma

Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema wizara hiyo kupitia tume imeendelea kuimarisha misingi ya utawala bora katika vyama vya ushirika ili kukabiliana na viongozi wabadhirifu wa vyama hivyo.

Bashe amesema hayo akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Amina Makilagi (CCM), aliyetaka mkakati wa serikali kuhakikisha vyama vya ushirika vinaimarika na kuleta tija.

Akijibu swali hilo Bashe amesema ushirika ni utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015-20 Ibara ya 29 katika vifungu vya f, g, na  ushirika ndiyo chombo pekee katika kumkwamua mkulima mdogo kupitia kuungana kutengeneza chombo imara cha kuwatetea.

“Wizara inatambua mapungufu yaliyopo sasa katika vyama vya ushirika vya mazao mbalimbali ikiwamo, pamba, kahawa, miwa na ufuta, ambapo baadhi ya viongozi wamekuwa wakifanya vitendo visivyofaa ikiwamo ubadhirifu hali iliyosababisha wakulima kutoaminika miongoni mwa wanachama walio wengi,” amesema Bashe.

Pamoja na mambo mengine, amesema wizara yake kupitia tume imeendela kuimarisha misingi ya utawala bora kwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara walau mara mbili kwa mwaka na ukaguzi wa mwisho wa kusimamia uchaguzi wao

“Aidha wizara inafanya tatmini ya ushirika kwa kuangalia muundo wake usimamizi wa rasirimali zake na wanachama ili kuleta tija kufanya uwe wa kibiashara zaidi kuliko udalali.

“Mikakati mingine ni kuhamasisha makundi mbalimbali hususani vijana ambapo tunawashauri kujiunga au kuanzisha vyama vya ushirika ili kuongeza idadi ya wanachama, kuhamasisha vyama vya ushirika vya akiba na mikopo yaani Saccoss kwenye vyama vya ushirika ili kuwajengea wakulima tabia ya kuweka na kupata mikopo yenye masharti nafuu,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles