25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Bashe: Hatutashusha bei ya mazao

Anna Potinus

Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema serikali haina mpango wa kupunguza bei za mazao ya wakulima badala yake watahamasisha Watanzania kuongeza uzalishaji ili bei ya mazao hayo iweze kushuka.

Ametoa kauli hiyo bungeni leo Jumatatu Novemba 11, katika kipindi cha maswali na majibu alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Busega, Dk. Raphael Chegeni aliyehoji mkakati wa serikali katika kupunguza gharama za bei ya vyakula.

“Sasa hivi bei ya vyakula inazidi kupanda na ukiangalia wananchi wengi wanaadhirika na hali hii, gunia la mahindi sasa ni karibu Sh. 100,000 je serikali ina mkakati gani wa kupunguza gharama hizi kwa wananchi,” – alihoji Dk. Busega.

Akijibu swali hilo Bashe amesema msimamo wa serikali ni kutokuingilia kushusha bei ya mazao kwa kuwa wakulima wameshapata hasara na hivyo watapunguza gharama za uzalishaji na kuruhusu ushindani katika soko.

“Hatutaingilia kupunguza bei ya mazao kwasababu wakulima wa nchi hii kwa muda mrefu wamepata hasara, huu ni msimamo wa serikali na ieleweke hivyo, njia ya pili tunahamsisha Watanzania kuongeza uzalishajikwani supply ikiwa kubwa demand ikiwa ndogo mazao yatashuka bei.

“Ni bunge hili hili mwaka jana wakati bei ya mahindi kwa mkulima ilikuwa sh. 150 wakasema kwanini tunafunga mipaka, sisi kama serikali hatua tunazozichukua kupunguza gharama za bei sokoni ni pamoja na kupunguza gharama za uzalishaji, kuruhusu soko kushindana, kwahiyo hatutaingilia kushusha bei, tunayo National Food Reserve Agency na niwaambie wabunge na wakuu wa mikoa pale wanapoona kuna upungufu wa mazao ya chakula sokoni wawasiliane na mawakala hao ili wasambaze chakula katika maeneo hayo,” amesema Bashe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles