27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Bashe awaonya wasambazaji viatilifu vya pamba

Derick Milton, Simiyu

Naibu Waziri wa Kilimo, Hussen Bashe amesema wamepata taarifa kuwa baadhi ya wasambazaji  waliopewa dhabuni ya kusambaza viuatilifu vya kuua wadudu kwenye zao la pamba wanaihujumu serikali.

Bashe amesema kuwa wamegundua wasambazaji hao wamekuwa wakiuzia serikali dawa hizo kupitia bodi ya pamba kwa bei kubwa kuliko wanavyowauzia watu wenye maduka ya kuuza viuatilifu hivyo.

Ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akipokea chupa 13,000 za viuatilifu vya pamba kutoka bodi ya pamba kwa ajili ya kuwapatia wakulima wa Mkoa wa Simiyu.

Bashe amesema kuwa wamegundua kuwepo kwa hujuma hizo, kwani viuatilifu hivyo vinavyouzwa kwenye maduka hayo bei yake imekuwa rahisi, kuliko vinavyouzwa na bodi ya pamba nchini.

Kutokana na hali hiyo Naibu Waziri huyo ameiagiza bodi ya pamba, kufanya operesheni kali kwenye maduka yote yanayouza dawa hizo kuangalia kama bei ya viuatilifu inayotumika inalingana na ile ambayo wanatumia bodi.

“Hatuwezi kuwa na wasambazaji wa aina hii, waliomba wenyewe tukawapa masharti, lazima wayatekeleze, hatuwezi kuendelea kumkandamiza mkulima, bodi ya pamba ifanye opereisheni kila duka kuangalia bei za uko,” amesema Bashe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles