23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

BASHE AITAKA SERIKALI KUFUTA KODI YA TENDE

Ramadhan Hassan, Dodoma

Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM) ameibana Serikali akiitaka kuondoa kodi ya tende katika mfungo wa Ramadhani ambao Waislamu kote duniani hufunga.

Akiomba mwongozo bungeni jijini Dodoma leo Mei 7, Bashe amedai: “Naomba kutumia kanuni ya 69 kama utaridhia ili angalau tuweze kuahirisha bunge angalau kwa dakika 30 tuweze kujadili jambo moja tu kwamba mwezi wa Ramadhani unakaribia na kama alivyoanza kusema Mheshimiwa Nkamia (Juma) bei ya mafuta ya kula imepanda, bei ya Sukari imepanda.

“Lakini Nchi zilizotuzunguka zimefuta kodi katika moja ya chakula ambacho huliwa sana mwezi wa Ramadhan na Waislamu na ni Sunna wakati wa kufuturu tende, kama utaridhia tuahirishe angalau kwa nusu saa Bunge lijadili tuweze kufanya azimio la kuitaka Serikali ifute kodi hiyo”.

Akijibu mwongozo huo Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema suala hilo Serikali italiangalia ili Bunge na Serikali iweze kupata thawabu kutokana na kuondoa kodi katika tende.

“Suala la tende tuzungumza na waziri na kuna kikao tulikifanya juzi kwa sababu hakikuwepo katika sheria yetu tuliyopitisha baada ya kuona lile tangazo la nchi  jirani ndiyo likawa linazunguka, tutalipeleka ili tumshawishi ili katika kipindi hiki Bunge na nchi tuchume thawabu,” amesema Mwijage.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,226FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles