30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Bashe aeleza mikakati kusaidia wakulima wa tumbaku

RAMADHAN HASSAN-DODOMA

SERIKALI imesema imefanya mazungumzo na Kampuni ya British American Tobacco Ltd ambayo imeonesha nia ya kununua kilo milioni nane za tumbaku inayozalishwa nchini.

Hayo yalielezwa bungeni jana na Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe wakati akijibu swali la Mbunge wa Urambo, Margaret Sitta (CCM) ambaye alisema licha ya juhudi za Serikali kumsaidia mkulima wa tumbaku, bado zipo changamoto za kutopata makisio na pembejeo kwa wakati na masoko ya uhakika.

Alihoji, Serikali ina mikakati gani ya kuondoa changamoto hizo ili mkulima ajiendeleze kiuchumi.

Akijibu swali hilo, Bashe alisema ili kuhakikisha wawekezaji wa tumbaku waliopo nchini wanaendelea kuongeza uwekezaji, Septemba, 2019 Wizara ya Kilimo ilikutana na kampuni za wanunuzi wa tumbaku kwa lengo la kujadili na kupata ufumbuzi wa changamoto zilizopo.

Alisema kutokana na kikao hicho, ilikubalika kuondoa kesi zilizofunguliwa na Tume ya Ushindani na kufanya makubaliano ya kirafiki.

Vilevile, Serikali italipa marejesho ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa kiasi halali ambacho inadaiwa.

Alisema Serikali imeendelea kuchukuwa hatua mbalimbali ili kuondoa changamoto kwenye tumbaku.

Alieleza katika msimu wa kilimo wa 2019/20 makisio ya uzalishaji wa tumbaku ya kilo 42,225,985 yalitolewa Julai na Kampuni za Alliance One Tobacco Tanzania Limited , Japan Tobacco International Leaf Services na Premium Active Tanzania Limited.

”Kutolewa mapema kwa makisio hayo kumewezesha vyama vya ushirika vya wakulima wa tumbaku kuagiza mbolea kwa wakati. Mahitaji ya mbolea kwa zao la tumbaku ni tani 14,951 za mbolea ya kupandia aina ya NPK 10:18:24 na tani 3,139 za mbolea ya kukuzia aina ya CAN (27%).

Mbolea yote imekwisha pokelewa nchini na usambazaji unaendelea kwenye vyama vya msingi. Kwa Wilaya ya Urambo hadi kufikia Oktoba 31, 2019  tani 1,774 zimesambazwa kati ya mahitaji ya tani 2,160 yambolea sawa na asilimia 82.13.

Alisema ili kuhakika, Serikali inaendelea na mazungumzo ili kufungua soko la tumbaku katika nchi wanachama wa COMESA (Algeria, Misri na Sudan), ambao niwateja wakuu wa Tumbaku ya Moshi inayozalishwa nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles