26 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

BASATA YAFUNGUKA KUTOFANYIKA MISS TANZANIA

NA CHRISTOPHER MSEKENA

TUKIWA  ukingoni mwa mwaka 2017, utakumbuka kuwa shindano kubwa la urembo nchini, Miss Tanzania halijafanyika kama ilivyo kawaida yake kiasi cha Baraza la Sanaa la Taifa  (Basata) kutoa taarifa yake juu ya ukweli wa kutofanyika kwa shindano hilo.

Katika barua yake kwa vyombo vya habari, Basata ilisema baraza limekuwa likifuatilia kwa umakini mwenendo wa shindano la Miss Tanzania na waandaaji wake, Kampuni ya Lino International Agency katika kuhakikisha taratibu, kanuni na miongozo ya kuendesha matukio ya sanaa nchini inazingatiwa.

Hivi karibuni Kampuni ya Lino wametoa taarifa za kutofanyika kwa mashindano ya Miss Tanzania mwaka 2017 ambapo pamoja na sababu hizo ni pamoja na kukosa wadhamini, wametaja kucheleweshewa kibali na Basata, kama sababu ya kutofanyika kwa shindano hili msimu wa mwaka 2017.

“Tunapenda kueleza kwamba sababu iliyotolewa na Lino si ya kweli na pengine imetengeneza kuficha uhalisi wa changamoto za shindano hili ambapo mara zote Basata na hivi karibuni Waziri mwenye dhamana na sekta ya sanaa, Dk. Harrison Mwakyembe amezieleza na kuzitolea maagizo, Basata kama mtoa vibali limeshangazwa na kutofanyika kwa shindano msimu huu maana lilishatoa vibali vya muda kwa Lino ili kufanya shindano hili sambamba na kuandaa mshiriki wa Miss World lililofanyika Sanya, nchini China,” ilisema taarifa hiyo

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles