Brighiter Masaki
BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA), limempongeza mbunifu wa mavazi nchini, Ally Rehmtullah kwa kuonyesha juhudi za kuwapa sapoti wabunifu wenzake katika kufikia malengo ya Kimataifa.
Afisa sanaa wa baraza hilo, Vivian Sharua ameliambia MTANZANIA kuwa Rehmtullah amekuwa mstari wa mbele katika kutangaza vazi la kitenge na kuwaleta wawekezaji kwenye tasnia ya mitindo nchini. “Wabunifu
wasiwe waoga katika kutumia fursa unapoiona unatakiwa kuichangamkia na kuacha na kubweteka. Ally ametoa fursa kwa wabunifu kuuza nguo zao, kujifunza kushona na kupata masoko lakini wamejitokeza wabunifu wachache kwenye fursa hiyo,” alisema Vivian.