25.5 C
Dar es Salaam
Thursday, September 28, 2023

Contact us: [email protected]

Basata kutoa tamko kwa wasanii, studio zisizosajiliwa

mungerezaNA GLORY MLAY

BARAZA la Sanaa la Taifa (Basata), leo linatarajiwa kutoa tamko kuhusu wasanii na studio zote zinazojishughulisha na muziki bila kusajiliwa na kuwa na vibali vya baraza hilo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka baraza hilo, tamko hilo litatolewa katika ofisi zake zilizopo Ilala, Bungoni jijini Dar es Salaam.

Kingine kitakachotolewa tamko na baraza hilo ni wasanii wote wanaoshiriki matukio ya sanaa bila kusajiliwa kwa kuwa wanatakiwa wawe wamesajiliwa na Basata na kufuata taratibu zote husika.

Hivi karibuni Baraza hilo lilipokutana na viongozi, wanachama na wadau wa mashirikisho ya sanaa nchini walijadili umuhimu wa wasanii kujiunga na mashirikisho ya sanaa nchini ili kuweza kusogeza mbele sanaa kwa pamoja.

Baada ya uchaguzi na kupatikana kwa viongozi mbalimbali wa mashirikisho hayo baadhi ya wasanii wameanza kujiunga nayo jambo ambalo linaonyesha mabadikliko ya matamko mbalimbali ya baraza hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,750FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles