29.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 1, 2023

Contact us: [email protected]

Barrick yaadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa kutoa msaada wa vifaa Hospitali ya Mwananyamala

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani Machi 8, Wafanyakazi Wanawake wa kampuni ya Barrick  kutoka ofisi ya Dar es Salaam wametembelea hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala na kukabidhi vifaa mbalimbali vya kusaidia matibabu vilivyotolewana kampuni pia walipata fursa ya kutembelea wodi ya wazazi ya hospitali hiyo.

Meneja Mawasiliano wa Barrick nchini, Georgia Mutagahywa (wa tatu kushoto) akibadilishana mawazo na Katibu wa afya wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala Lilian Mwanga baada ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya matibabu vilivyotolewa na Barrick katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. Wengine pichani ni wafanyakazi wa Barrick na hospitali ya Mwananyamala.

Akiongea na uongozi wa Hospitali hiyo leo Machi 7, 2023, Meneja Mawasiliano wa Barrick nchini (Corporate Communications and Country Liasion Manager), Georgia Mutagahywa, amesema katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani mwaka huu, pamoja na kampuni kuwa na programu mbalimbali za ndani pia imeandaa programu za kusaidia jamii .

Amesema Barrick, imekuwa ikitoa kipaumbele kuunga mkono jitohada za Serikali katika kuboresha sekta ya afya nchini ambapo kupitia fedha za uwajibikaji kwa jamii imeweza kujenga vituo vya afya katika maeneo yanaozunguka migodi yake ya Bulyanhulu na North Mara.

Katibu wa Afya wa Hospitali hiyo,Lilian Mwanga. aliishukuru Barrick kwa msaada huo sambamba na baadhi ya wafanyakazi wake kujitolea muda wao kutembelea hospitali na  kutembelea wagonjwa walioalazwa hospitalini hapo ikiwemo Wanawake waliolazwa katika wodi ya wazazi..

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,404FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles