Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani Machi 8, Wafanyakazi Wanawake wa kampuni ya Barrick kutoka ofisi ya Dar es Salaam wametembelea hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala na kukabidhi vifaa mbalimbali vya kusaidia matibabu vilivyotolewana kampuni pia walipata fursa ya kutembelea wodi ya wazazi ya hospitali hiyo.
Akiongea na uongozi wa Hospitali hiyo leo Machi 7, 2023, Meneja Mawasiliano wa Barrick nchini (Corporate Communications and Country Liasion Manager), Georgia Mutagahywa, amesema katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani mwaka huu, pamoja na kampuni kuwa na programu mbalimbali za ndani pia imeandaa programu za kusaidia jamii .
Amesema Barrick, imekuwa ikitoa kipaumbele kuunga mkono jitohada za Serikali katika kuboresha sekta ya afya nchini ambapo kupitia fedha za uwajibikaji kwa jamii imeweza kujenga vituo vya afya katika maeneo yanaozunguka migodi yake ya Bulyanhulu na North Mara.
Katibu wa Afya wa Hospitali hiyo,Lilian Mwanga. aliishukuru Barrick kwa msaada huo sambamba na baadhi ya wafanyakazi wake kujitolea muda wao kutembelea hospitali na kutembelea wagonjwa walioalazwa hospitalini hapo ikiwemo Wanawake waliolazwa katika wodi ya wazazi..