28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Barnabas, Mc Pilipili kuhimiza wasichana wapende ufundi

Barnaba akitumbuizaAsifiwe George na Zamda Biwi (RCT)

TAMASHA la Binti Thamani linalotarajiwa kufanyika leo katika ukumbi wa King Solomon jijini Dar es Salaam, litanogeshwa na burudani kutoka kwa mwimbaji na mpiga gitaa, Elias Barnaba (Barnaba), bendi ya Classic na mchekeshaji mahiri, Mc Pilipili.

Mkurugenzi wa Don Bosco, Celestine Kharkongor, alisema tamasha hilo lililoandaliwa na Don Bosco litawaunganisha vijana wa kike zaidi ya 1,000 kutoka shule mbalimbali za sekondari jijini Dar es Salaam likiwa na lengo la kuhamasisha wasichana kupenda mafunzo ya ufundi stadi.

Alisema kupitia mafunzo hayo yatawawezesha wasichana kuwa mabalozi wazuri katika kuhamasisha wasichana wengi zaidi wapende mafunzo hayo.

“Idadi kubwa ya wavulana wanachangamkia mafunzo hayo lakini wasichana wamekuwa wakiyakimbia hivyo wazazi na walezi washirikiane nasi pamoja katika harakati ya kuhamasisha wasichana wayapende kwa kuwa ndiyo tegemeo la jamii yetu,” alimaliza Kharkongor.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles